|
Wasimamizi wa Redio za Jamii wakisikiliza kwa
makini wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam.
|
|
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi.
Zulmira Rodrigues, akiwagawia wasimamizi wa redio za jamii katiba
iliyopendekezwa iliwekwa kwa njia ya sauti.
Wakurugenzi na Viongozi mbalimbali wa Radio za Jamii wamethibitisha
kupokea na kuanza kurusha Katiba Inayopendekezwa kwa njia ya sauti, makala na
michezo ya radio iliyoandaliwa na Kampuni ya Focus Media na COMNETA zenye
maudhui ya katiba inayopendekezwa.
Wakizungumza na Focus Media ambao ndio waandaaji na wasambazaji wamekiri
kwamba wamepokea kwa wakati muafaka, kwani hawakuwa na chanzo sahihi cha kupata
maudhui yanayohusu elimu ya uraia na uchaguzi mkuu na kura ya maoni.
Baadhi ya wasimamizi wa Radio zilizo katika mtandao wa radio za kijamii
Community Media Network of Tanzania ambao wamethibitisha kupokea vitendea kazi
hivyo ni Bw. Ali Khamis Mtwana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tumbatu Island Community
Radio, Bw. Anton Masai Triple A FM Arusha, Dr. Lazaro Ole Mongoi Mkurugenzi
Mtendaji wa IDEA Radio, Henry Bernard, Adelina Lweramla, Jackson Mollel, wa ORS
FM Arusha, Edwin Mpokasye, Radio Fadhila, Mkurugenzi Radio Kwizera- Ngara.
Vipindi vinapokuwa vikiruka hewani wasikilizaji wamekuwa wakishiriki kwa
kupiga simu na kuuliza maswali ilikuelewa zaidi Katiba Inayopendekezwa.
Wengine wanapiga simu kupongeza na mnamichezo ya radio ilivyoratibiwa
vizuri na ikielimisha jamii juu ya mambo mbalimbali muhimu.
Source:-Dewji
Blog
http://myradiostream.com/focusradiotz www.katibainayopendekezwa.or.tz www.facebook.com/KatibaInayopendekezwaTanzania Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |





No comments:
Post a Comment