|
Jinamizi la
ajali limeendelea kugharimu maisha ya Watanzania, baada ya jana April 09, 2015
,Watu 12 kufa katika ajali mbili tofauti zilizohusisha magari manne katika
mikoa ya Tanga na Morogoro,Nchini Tanzania.
Ajali hizo
zimetokea takribani mwezi mmoja tangu kutokea kwa ajali nyingine ya basi
iliyoua abiria 43 mkoani Iringa.
Katika ajali
mkoani Tanga iliyoua watu 10 katika eneo la Mkata katika Kijiji cha Mbweni
wilayani Handeni Mkoani Tanga, magari matatu yakiwemo gari dogo, mabasi ya NGORIKA
na RATCO, yaligongana majira ya saa 5 asubuhi na kusababisha vifo na majeruhi.
Polisi
mkoani Tanga kupitia Kaimu Kamanda wake, Juma Ndaki amethibitisha tukio hilo na
kusema ajali hiyo iliyotokea katika barabara ya Dar es Salaam kwenda Tanga na
Arusha.
Kwa mujibu
wa Kamanda Ndaki, gari dogo aina ya Toyota Passo lenye namba za usajili T 628
CXE lililokuwa likiendeshwa na Baba mzazi wa binti mwenye matatizo ya akili
aliyekuwa akipelekwa hospitali ya Rutindi, Korogwe, ndilo chanzo cha ajali,
kwani dereva wake ailijaribu kulipita lori ili amwahishe binti yake hospitali,
ndipo akajikuta anasababisha ajali hiyo.
Anasema
wakati gari hilo dogo likijaribu kulipita lori, lilikutana uso kwa uso na basi
RATCO lenye namba T 274 DCP na ndipo dereva wa basi hilo akajaribu kulikwepa na
kisha kukutana uso kwa uso na basi la NGORIKA lenye namba T 770 BKW na
kusababisha ajali iliyoua watu wanane wa basi la NGORIKA akiwemo dereva wake,
na wawili, Baba na bintiye waliokuwa kwenye gari dogo. |
No comments:
Post a Comment