|
Hali
halisi ya Ubungo ilivyokuwa asubuhi leo April 10, 2015.
|
|
Umati wa
watu ukimshuhudia jamaa mmoja aliyekuwa akitoa ibada fupi ya kuombea nchi
kuhusiana na mgomo wa madereva ambao ni wa nchi nzima eneo la Ubungo.
MADEREVA wa mabasi ya mikoani na daladala wa
jijini Dar es Salaam leo April 10,2015 wamefanya mgomo kupinga agizo la Mamlaka ya Kudhibiti Usafiri wa
Majini na Nchi Kavu (Sumatra) lililowataka kwenda kusoma katika Chuo cha
Usafirishaji (NIT).
Mwandishi
wetu pia aliweza kufika eneo la Stendi ya Ubungo na kujionea hali ilivyokuwa
asubuhi na kuzungumza na baadhi ya madereva ambao walikuwa na kauli
tofautitofati kuhusiana na mgomo huo.
Mmoja wa
madereva ambaye alijitambulisha kwa jina la Ally Abdallah Shalon anayefanya
kazi zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma, alisema kuwa sababu kubwa ya
kutokufanya shughuli zake ni kutokana na kikao ambacho walipanga kukifanya leo
kujadili agizo la Sumatra lililowataka waende shule kusoma.
Dereva
mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Khamis anayefanya shughuli zake
kati ya Mwanza na Dar es Salaam alisema sababu iliyomfanya agome ni kupinga
sheria mpya ya Sumatra iliyopitishwa na jeshi la polisi kuwataka madereva wote
wa abiria (Pasangers Services Vehicle) kwenda kusoma kozi ya miezi miwili kwa
gharama ya shilingi laki tano.
Khamisi
alisema sheria hiyo inawabana sana madereva kwani moja kati ya vipengele vya
sheria hiyo imeeleza kuwa, dereva yeyote atakayekamatwa akiwa amezidisha mwendo
kasi hakuna faini yoyote bali unapelekwa mahabusu kwa muda wa siku kumi na nne
baada ya kumaliza siku hizo, anapelekwa mahakamani kujibu shitaka
linalomkabili.
“Hii sheria
inatubana sana, mtu ukihitaji kubadilisha leseni yako ikipitwa na muda
unatakiwa kurudia tena kwenda kusoma darasani kwa muda wa wiki mbili kwa ada
isiyopungua laki tano na kuendelea kitu ambacho kinatuumiza sisi madereva,”
alisema Khamis.
MUSOMA
Huko Musoma, abiria zaidi 1000 waliokuwa wakisafiri kutoka Musoma kwenda Dar es Salaam kupitia mkoani Mwanza na Shinyanga na wale wa kwenda mpakani mwa Tanzania na Kenya pamoja na wa ndani ya Mkoa wa Mara wameshindwa kusafiri baada ya madareva kuitisha mgomo leo.
KIBAHA
Zaidi ya mabasi 10 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa yamekwama huko Kibaha mkoani Pwani kutokana na mgomo wa madereva leo.
BUKOBA
Mabasi yote ya abiria yaliyotoka Bukoba Mjini leo asubuhi kuelekea Dar, Mwanza na kwingineko yamezuiliwa wilayani Muleba kutokana na mgomo wa madereva unaoendelea nchini kote. Abiria wamerudi mjini Bukoba kurudishiwa nauli zao na kuahirisha safari.
(PICHA/HABARI:
DENIS MTIMA/GPL)
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|





No comments:
Post a Comment