LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Hiki ndicho Azam FC,Simba SC na Mbeya City walichokivuna katika mechi zao za April 25, 2015.! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 26, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Hiki ndicho Azam FC,Simba SC na Mbeya City walichokivuna katika mechi zao za April 25, 2015.!

Mabingwa Watetezi wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara, Azam FC hapo Jana April 25, 2015  wameendeleza matumaini yao finyu ya kutetea Taji lao la Ligi Kuu Vodacom msimu huu 2014/2015 baada ya kuitwanga Stand United Bao 4-0 na Simba SC nao wanaendelea kuifukuza Azam FC ili kuipiku Nafasi ya Pili baada ya kuichapa Ndanda FC 3 - 0 huku Mbeya City ikijizatiti kwa kuiwasha Kagera Sugar 2-0.

 Kwa matokeo hayo ya mechi za jana Jumamosi April 25,2015, Azam FC kwa ushindi huo inafikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 23, ikiwa nyuma ya Yanga SC yenye pointi 52 za mechi 23 na mbele ya Simba SC yenye pointi 41 za mechi 24. 

LIGI KUU VODACOM 2014/2015 RATIBA.

Jumapili Aprili 26,2015.

Mtibwa Sugar v Ruvu JKT

Tanzania Prisons v Mgambo JKT

Jumatatu Aprili 27,2015.

Yanga v Polisi Moro

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad