LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Simba SC washinda 4-0 kwa Okwi akipiga ‘hat-trick’ . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 22, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Simba SC washinda 4-0 kwa Okwi akipiga ‘hat-trick’ .

Mkali kweli; Emmanuel Okwi aliyepiga magoti akishangilia moja ya mabao yake leo April 22,2015 wakati wa mchezo wa Ligi kuu Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezaji  Emmanuel Okwi amepiga ‘hat-trick’ Simba SC ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Mgambo Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wekundu wa Msimbazi sasa wanatimiza pointi 38 baada ya kucheza mechi 23, maana yake wamerudi kwenye mawindo ya nafasi ya pili dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 42 za mechi 22.
Beki wa Simba SC, Mohammed Hussein 'Tshabalala' akimtoka beki wa Mgambo, Ramadhan Malima.

Timu mbili za mbili katika Ligi Kuu hucheza michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), bingwa akicheza Ligi ya Mabingwa na mshindi wa pili Kombe la Shirikisho.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

1 comment:

Post Bottom Ad