PICHA / AJALI SHINYANGA:-Watu 10 wapoteza maisha na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa katika ajali ya basi leo April 22,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 22, 2015

PICHA / AJALI SHINYANGA:-Watu 10 wapoteza maisha na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa katika ajali ya basi leo April 22,2015.


Basi la Unique Express baada ya kuinuliwa na kuondoa miili ya watu watatu waliokuwa wamenasa kwenye basi.

 Watu kumi wamepoteza maisha leo April 22, 2015 katika ajali iliyotokea katika kijiji cha ibingo kata ya Samuye mkoani shinyanga ajali iliyohusisha basi la UNIQUE lenye namba T 148 BKK na LORI la kampuni ya COCA COLA lenya namba za usajili T 207 BSA liliokua linakokota tela namba T 655 AJT.

Kwa maelezo ya abiria aliyenusurika katika ajali hiyo Kevin Moshi ameeleza Dereva wa gari hilo alikua anaendesha kwa mwendo kasi na walipofika katika eneo la Samuye wakakutana na Lori hilo likiwa katikati ya barabara na ndipo ajali ikatokea.




 Tela la lori la kampuni ya Coca cola lililokuwa linaelekea Shinyanga.

Naye Diwani wa Kata ya Samuye,Bw Amosi Shija amesema alishuhudia ajali hiyo baada ya kusikia kishindo kikubwa lakini basi hilo lilikua katika mwendo mkali hali iliyosababisha ajali kutokea baada Dereva wa basi kushindwa kupishana Lori hilo.

Miili ya marehemu ikiwekwa kwenye lori baada ya kutolewa kwenye basi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema watu tisa wamekufa hapo hapo na mtu mmoja amefariki wakati akipelekwa katika hospitali huku majeruhi 50  wakiwemo wanawake 13,wanaume 36 na mtoto mmoja  wa kiume wanapata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga. Aidha amewataka madereva kuendesha magari kwa kuzingatia sheria za barabara ili kuepusha ajali ambazo zimekua zikigharimu maisha ya watu.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio,Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


1 comment:

Post Bottom Ad