![]() |
|
MWANANCHI
Madaktari katika maeneo yaliyonufaika na bajaji za kubebea wagonjwa, wamelazimika kuwa madereva wa kuziendesha baada ya Serikali kushindwa kuajiri madereva. Mganga Mkuu wa hospitali ya Dodoma Dk. Ezekiel Mpuya alisema Mkoa wa Dodoma ulifanikiwa kupata bajaji 10 na kila Wilaya ilipatiwa mbili lakini zote hazina madereva. Dk Mpuya alisema madaktari hao licha ya kuziendesha bajaji hizo hukumbana na changamoto ya ubovu wa barabara unaowapa wakati mgumu pindi wanaposafirisha wagonjwa wanaopatiwa rufaa kwenda hospitali ya Mkoa wa Dodoma. “Wakati mwingine huwa zinafia njiani kutokana na ubovu wa barabara, kwa upande mwingine naweza kusema sio msaada sahihi ” Dk Mpuya. Ameiomba Seikali kuzipatia uwezekano wa magari ya wagonjwa hospitali hizo ili kuepuka adha wanayokumbana nayo sasa.
MWANANCHI
Uwezekano wa Kura ya Maoni kufanyika mwaka huu na hasa sambamba na Uchaguzi Mkuu, umeanza kujionyesha baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza zabuni za ununuzi wa vifaa vitakavyotumika kwenye shughuli hiyo, zikiwamo karatasi za kupigia kura. Kati ya matangazo hayo mawili, moja litakamilisha mchakato wa upokeaji maombi ya zabuni Mei 11, mwaka huu na nyingine kufungwa siku tisa baadaye. “Serikali ya Tanzania imetenga fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika mwaka wa fedha 2014/15. Imepanga kuwa sehemu ya fedha hizo zitatumika kugharamia ununuzi wa vifaa mbalimbali na huduma zisizo za kishauri kwa ajili ya Kura ya Maoni 2015,” inasomeka sehemu ya tangazo hilo. Katika matangazo hayo, NEC imetoa zabuni sita tofauti zitakazojumuisha ununuzi wa fulana na kofia, ununuzi wa bahasha zisizoweza kuchakachuliwa, uchapaji na uchapishaji wa karatasi za kupigia Kura ya Maoni. Wazabuni hao pia watatakiwa kutoa huduma mchanganyiko zinazojumuisha vifaa vya ofisini, vifaa vya kuhifadhia nyaraka na vitu mbalimbali pamoja na taa za chemli. Pia, wataiuzia NEC chemba za kupigia kura, wino maalumu, lakiri za masanduku ya kura na betri. Vilevile, Tume inataka wazabuni kufanikisha ununuzi wa kompyuta, skana, printa, modemu, projekta na mashine za kunakili. Huduma nyingine zinahusisha ununuzi wa vifaa mbalimbali vinavyotumika katika printa na mashine za kunakili. Katika tenda nyingine, NEC inatafuta kampuni itakayotoa huduma za kukodisha malori na magari madogo yenye uwezo wa ‘four wheel’ kwa ajili ya kubebea vifaa vya Kura ya Maoni katika kata mbalimbali. Hata hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema pamoja na maandalizi hayo, hadi sasa hakuna tarehe maalumu iliyokubaliwa kufanyika kwa Kura ya Maoni na kwamba nguvu zote zimeelekezwa kwenye uboreshaji wa Daftari la Wapigakura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR).....KUSOMA HABARI ZAIDI...BOFYA HAPA
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Friday, April 24, 2015
Home
HABARI
HABARIKA:-Madaktari wageuka Madereva wa Bajaji na Risasi zarindima msafara wa CHENGE ni Stori 9 kubwa MAGAZETINI leo April 24,2015.
HABARIKA:-Madaktari wageuka Madereva wa Bajaji na Risasi zarindima msafara wa CHENGE ni Stori 9 kubwa MAGAZETINI leo April 24,2015.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment