KILI MUSIC AWARDS 2014/2015:-Fahamu Majina rasmi ya wateule (nominees) wa vinyang’anyiro 32 vya tuzo za muziki Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 29, 2015

KILI MUSIC AWARDS 2014/2015:-Fahamu Majina rasmi ya wateule (nominees) wa vinyang’anyiro 32 vya tuzo za muziki Tanzania.

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na bia ya Kilimanjaro, leo April 29, 2015 imetangaza rasmi majina ya wateule (nominees) wa vinyang’anyiro 32 vya tuzo za muziki Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards).

Akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa bia ya Kilimanjaro, Bi. Pamela Kikuli alisema kuwa akademy ilikaa mwisho wa wiki iliyopita na kufanya kazi ngumu na nzito ya kupitia mapendekezo ya umma na hatimaye kuteua kwa njia ya kupiga kura.

“Zoezi la kupata wateule lilidumu kwa zaidi ya saa 18 kudhihirisha umahiri na kujituma kwa kundi la akademi,” alisema Kikuli.


Mchakato wa akademi ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala AUDITAX International ili kuhakikisha zoezi linafanywa kwa huru na haki.

Tanzania itapewa nafasi kuanza kupiga kura kwa kutumia njia zile ili kuchagua mshindi kwa kila kipengele.
 
Kura zitaanza kupigwa tarehe 5 Mei 2015 hadi Juni 5 2015. Njia za kupiga kura ni kama zifuatazo.

1.    Whatsapp: 0686 528 813

2.    SMS: 15415

3.    Mtandao: www.ktma.co.tz



Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad