FAHAMU HILI:-Ni Marais 8 Matajiri barani Africa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 24, 2015

FAHAMU HILI:-Ni Marais 8 Matajiri barani Africa.

Rais Jose Eduardo Dos Santos.

Kuna tafiti mbalimbali zilizowahi kufanywa, lakini leo nimekuja na hii list ya Marais nane wanaoongoza kwa kuwa na utajiri mkubwa zaidi ya wenzao Afrika.

 Ukiachilia mbali Marais wengi wa Afrika kupenda kukaa kwa muda mrefu madarakani lakini kuna hili la kujilimbikizia mali, wengine huzipata kabla ya kuwa marais lakini wengi wao huzipata wakati wanashikilia madaraka kwa kipindi chote wanapotawala nchi husika.

Bw.Jose Eduardo Dos Santos.

Ndiye Rais anayeongoza kwa utajiri Afrika kutoka Angola, aliingia madarakani mwaka 1979, ana utajiri wa dola bilioni 20.
Mohammed VI.

 Ni Mfalme wa Morocco ambaye amekaa madarakani kwa miaka 15 ,, ana utajiri wa dola bilioni 2.
Bw.Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

 Rais huyu wa Equatorial Guinea aliingia madarakani 1979, ana una utajiri wa dola milioni 600 licha ya wananchi wa nchi hiyo kuishi maisha ya kimaskini kutokana na uchumi wao kuwa chini.

Bw.Uhuru Kenyatta.

Ni Rais wa Kenya ambaye alichaguliwa mwaka 2011, ana utajiri wa dola milioni 500, mbali ya kuongoza nchi ana vyanzo mbalimbali vya utajiri ikiwa kuwa na hisa nyingi katika kampuni mbalimbali,benki na mahoteli makubwa ya kifahari.
Bw. Biya .

Ni Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982, ana utajiri wa dola milioni 200, unaambiwa ndiye rais anayetumia kiasi kikubwa cha pesa katika ziara zake kuliko marais wote duniani na hutumia euro 30,000 kwa siku katika ziara zake.
King Mswat III.

  Ni mfalwe wa Swazland akiwa na utajiri wa dola milioni 100, anashika nafasi ya 15 katika familia za kifalme tajiri duniani, Unaambiwa wake zake 13 hutumia zaidi ya dola milioni sita kufanya manunuzi yao pekee, pia Serikali yake hutenga bajeti ya dola milioni 61 kila mwaka kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Rais Idriss Derby.

 Yeye Ni Raisi wa Chad tangu mwaka 1990 na ana utajiri zaidi ya dola milioni 50.
Rais Robert Mugabe.

Ni rais wa Nchi ya Zimbabwe, ana zaidi ya miaka 26 akitawala nchi ya Zimbabwe, utajiri wake ni Dola milioni 10.

Source:-Milladayo.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad