PICHA / HABARI:-Kampuni ya TISA ACTION MART Yabomoa nyumba mjini Ngara Mkoani Kagera baada ya kuuzwa tangu 2013. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 14, 2015

PICHA / HABARI:-Kampuni ya TISA ACTION MART Yabomoa nyumba mjini Ngara Mkoani Kagera baada ya kuuzwa tangu 2013.

Na Shaaban Ndyamukama.

Mahakama ya ardhi ya Chato Mkoani Geita imetoa kibali kwa  kampuni ya TISA ACTION MART kubomoa nyumba ( Pichani ) ilioko katika kiwanja NO. 45 cha  Mactilida Kamala (73) kilichopo  mjini Ngara Mkoani Kagera baada ya  kuuzwa tangu 2013.

 Ubomoaji huo umefanyika leo April 14,2015 mjini Ngara chini ya usimamizi wa jeshi la polisi ambapo mmiliki wa kiwanja hicho Bw Charles Mkombo amesema anahitaji kujenga nyumba katika kiwanja hicho ili kufanya shughuli zake.

Bw Mkombo amesema alinunua kiwanja tangu Desemba mwaka juzi kwa shilingi  millioni 14 lakini mmiliki wa nyumba hiyo amekua akikaidi kuondoka ambapo alifungua kesi mahakama ya ardhi iliyoko wilayani chato ili kupata haki yake.

Aidha Bi Mactilida Kamala amekanusha kuhusu uuzaji wa kiwanja hicho na kwamba wana ukoo wenzake wamemzunguka na kukiuza  licha ya kusainishwa nyaraka mbalimbali kwa madai atapewa msaada   kutokana na kuwa  mjane.

Kwa upande wa  mtoto wa  Mactilida aliyejitambulisha kwa jina la Bashasha Kamala amelaani kitendo cha kubomoa nyumba ya mama yake na kwamba harakati za kuuzwa kwa kiwacha cha mama huyo yeye   hakuhusishwa.

Hata hivyo Bw Tuombe   Sempiga aliyekuwa na nyaraka za ununuzi wa kiwanja hicho nyingine zikiwa za mahakama ya ardhi ya Chato ambaye ni jirani na kiwanja hicho amesema manunuzi yalifanyika kihalali mbele ya ukoo wa mjane  huyo.

Madalali wa   kampuni ya TISA ACTION MART iliyo na makao makuu jijini Mwanza wakibomoa nyumba ilioko  kiwanja NO. 45  cha Mactilida Kamala (73) kilichopo  mjini Ngara mkoani Kagera baada ya kuamuliwa kuvunjwa na Mahakama ya Ardhi  wilayani Chato mkoani Geita tangu kiuzwe mwaka 2013.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad