Jeneza lenye mwili wa marehemu
Sylvestre Marsh likiingizwa kaburini kwenye makaburi ya Igoma, mkoani Mwanza.
|
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa
Mulongo akiaga mwili wa marehemu Marsh.
|
Vijana walio katika Kituo cha soka cha Marsh Academy kilichokuwa kikiongozwa na marehemu wakishusha jeneza la mwalimu wao kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Milongo tayari kwa kuaga. |
Mke wa marehemu (wa pili kushoto)
akilia kwa simanzi. Wa kwanza kushoto ni binti wa marehemu aitwaye Anna Marsh
na kijana wake Wyne Marsh (wa tatu kushoto).
|
Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo
viongozi wa serikali wakishiriki kumuaga marehemu Marsh.
|
Mmoja wa wadhamini wa kituo cha
marehemu kutoka nchini Ujerumani akitoa salamu za rambirambi.
|
Nahodha wa timu ya vijana ya U-16
katika kituo cha marehemu akisoma historia ya Academy yao.
|
...Nahodha huyo akikakabidhi historia
hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
|
Sehemu ya
waombolezaji waliohudhuria zoezi hilo.
MAJONZI,
vilio na simanzi vimetawala wakati kocha wa zamani wa timu ya Taifa 'Taifa
Stars', Sylvestre Marsh alipokuwa akiagwa leo March 17,2015, na kisha kuzikwa katika makaburi
ya Igoma, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Kocha Marsh
alifariki dunia Jumamosi ya March 14,2015,iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
alipokuwa amelazwa akitokea Mwanza baada ya hali yake kuwa mbaya.
Mamia ya watu
wakiwemo viongozi wa kiserikali, wadau wa soka, wanasoka na mashabiki
wamehudhuria mazishi hayo yaliyoanzia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Milongo
ambapo marehemu Marsh na vijana wake walikuwa wakifanyia mazoezi.
Zoezi la
kuaga mwili wa marehemu lilianza asubuhi katika uwanja huo baada ya mwili
kuwasili kutoka katika Hospitali ya Seketule ulipokuwa umehifadhiwa.
Vijana
waliokuwa wakifundishwa na Marsh katika Kituo cha soka cha Marsh Academy ndiyo
waliopewa jukumu la kubeba jeneza la mwalimu wao.
Wanasoka wa
zamani akiwemo Edibily Jonas Lunyamila na Fumo Felician ambao waliwahi kucheza
soka na marehemu kabla ya kuwa kocha walimwaga machozi wakati wa zoezi la
kumuaga mwenzao.
Wasanii
wakiwemo Steve Nyerere na H-Baba nao wameungana na waombolezaji kumuaga mwalimu
Marsh.
Sylvestre
Marsh aliyezaliwa miaka 55 iliyopita, licha ya kuwa kocha msaidizi wa Taifa
Stars tangu enzi za Marcio Maximo hadi Kim Poulsen, pia aliwahi kuwa kocha wa
timu kadhaa zikiwemo Azam FC na Kagera Sugar.
(PICHA ZOTE
NA JOHNSON JAMES / GPL, MWANZA)
UNGANA NASI KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment