VPL 2014/2015:-Baada ya Mechi 13, Yanga SC wana Pointi 25 wakishinda leo Februari 08,2015 dhidi ya Mtibwa Sugar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 08, 2015

VPL 2014/2015:-Baada ya Mechi 13, Yanga SC wana Pointi 25 wakishinda leo Februari 08,2015 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mrisho Ngassa kushoto akishangilia Simon Msuva baada ya kufunga leo Februari 08,2015 kwenye Mechi ya Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara.

 Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea hii leo Februari 08,2015 kwa  mchezo mmoja uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ukiwakutanisha wenyeji Yanga SC na Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.

Katika mchezo huo Yanga SC  waliibuka na ushindi wa goli 2-0 katika mchezo ambao mabao yote mawili Yalifungwa kupitia kwa kiungo mshambuliaji  Mrisho Khalfan Ngassa ambaye alifunga mabao mawili baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa Liberia, Kper Sherman.

Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Yanga SC  baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Coastal Union kwa bao moja.

Matokeo haya yanawafanya Yanga SC Baada ya Mechi 13, wapande  kwenye kilele cha Ligi kuu ya Tanzania bara 2014/2015 wakiwa na idadi ya pointi 25 wakiwazidi Mabingwa watetezi Azam FC kwa pointi tatu,wenye Pointi 22 kwa Mechi 12.

Mshambuliaji wa Yanga SC, Amisi Tambwe akimruka kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed aliyedaka mpira chini. Kushoto ni beki Salim Mbonde.
Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi akimdhibiti beki wa Yanga SC, Mbuyu Twite.

Ligi soka Tanzania bara itaendelea Jumatano Februari 11,2015 kwa Mechi 3 ambapo Azam FC watacheza na Mtibwa Sugar huko Azam Complex Jijini Dar es Salaam wakati Yanga SC pia watakuwa Jijini Dar es Salaam Uwanja wa Taifa kucheza na Ndanda FC huku huko Tanga Mgambo JKT watacheza na Simba SC.

RATIBA VPL 2014/2015.

Jumatano Februari 11,2015.

Azam FC v Mtibwa Sugar 

Mgambo JKT v Simba SC

Yanga SC v Ndanda FC

Jumamosi Februari 14,2015.

Polisi Moro v Simba   SC
       
Ndanda FC v Mtibwa Sugar
                  
Coastal Union v Mbeya City 
                 
Stand United v Mgambo JKT
                 
Kagera Sugar v JKT Ruvu   
         
MSIMAMO.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
 A
 
GD
PTS
1
Yanga
13
7
4
2
15
7
 
8
25
2
Azam FC
12
6
4
2
17
10
 
7
22
3
Polisi Moro
14
4
7
3
12
11
 
1
19
4
JKT Ruvu
14
5
4
5
14
14
 
0
19
5
Ruvu Shooting
14
5
4
5
10
11
 
-1
19
6
Mtibwa Sugar
12
4
6
2
13
9
 
4
18
7
Coastal Union
14
4
6
4
10
9
 
1
18
8
Kagera Sugar
14
4
6
4
11
11
 
0
18
9
Simba
13
3
8
2
13
11
 
2
17
10
Mbeya City
13
4
4
5
9
11
 
-2
16
11
Ndanda FC
14
4
3
7
13
18
 
-5
15
12
Mgambo JKT
12
4
2
6
6
11
 
-5
14
13
Stand United
14
2
6
6
9
17
 
-8
12
14
Tanzania Prisons
13
1
8
4
10
12
 
-2
11

MATOKEO- MECHI ZILIZOPITA.

Jumamosi Februari 7,2015.

Polisi Moro 2 Azam FC 2   
          
Coastal Union 0 Simba 0

Prisons 1 Ruvu Shootings 1   
               
JKT Ruvu 1 Mbeya City 1 
 
Ndanda FC 1 Stand United 1  
              
Kagera Sugar 1 Mgambo JKT 0 


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad