|
Akizungumza wakati akijibu maswali mbalimbali katika
mahojiano maalumu, mwanamuziki huyo pia alielezea mambo mengi kuhusu muziki
wake na hii ni sehemu ya mahojiano hayo;-
Swali: Nini chanzo cha bifu lako na Diamond?
Ali Kiba: Hakuna kiini kwa sababu nadhani hayo mimi aaah.…Kiukweli haya tuliyamalizaga
muda mrefu …Labda watu wahisi kwamba kipindi kile alichonifuta katika wimbo
wake (alisema bila kufafanua jina la wimbo) na yeye alivyosema kwamba nimemfuta
katika wimbo wangu ‘Single Boy’, mimi sijawahi kurekodi na Diamond katika wimbo
wangu hata mmoja na huo niliimba na Lady Jaydee.
Yeye ndiye aliyesema kwamba nilimfuta katika wimbo ule, ila
ukweli ni kwamba hatukuwahi kuingia pamoja studio, nilimshauri tufanye wimbo
mwingine lakini siyo ule kwa sababu nimeshaimba na Lady Jay Dee.
Swali: Umeshawahi kuwa karibu na Diamond?
Ali Kiba: Hapana yeye ndiyo alishawahi kuwa na ukaribu na mimi.
Swali: Unaweza kufanya kolabo na Diamond?
Ali Kiba: Ngoja nikwambie ukweli, sidhani kama ninaweza kuja
kufanya kolabo na Diamond, ila nikipata wimbo ambao nadhani kwamba anastahili
kuwapo, kiukweli nitamshirikisha lakini kama hastahili haitawezekana.
Kwa sababu kila wimbo unajielezea, kwa mfano kama mtu anataka
kufanya Zouk akimtafuta Stara Thomas itawezekana kwani hayo ndiyo mambo yake,
kwa hiyo kama nikitaka kufanya naye wimbo ambao nitaona kwamba unafaa
nitamfuata na nitamweleza.
Swali: Utofauti kati yako na Diamond ni upi?
Ali Kiba: Mimi naimba muziki mzuri na nina ‘hit song’, naye Diamond anaimba ‘hit
song’, unaposema mimi sina hit song wakati mimi nina nyimbo nyingi kushinda
yeye unakuwa unakosea, tangu nimeanza kuimba ni nyimbo mbili tu hazijawahi kuwa
hit ikiwamo ‘My Everything’ na ‘Mali Yangu’ lakini nyingine zote zilivuma tangu
nianze kufanya muziki.
Swali: Inasemekana katika Tamasha la TigoMusic kuna hirizi
zilionekana Uwanja wa Leaders na wewe na Diamond mnatuhumiwa kuhusika,
unalizungumziaje?
Ali Kiba: Yaani Mungu mmoja sina imani hiyo kabisa na mimi naamini Mungu na mambo
ya hirizi na mimi ni tofauti. Nadhani watu wanasema hivyo kwa sababu wanadhani
kwamba kuna bifu. Binafsi sina bifu na msanii yeyote labda kama wanaweza kuwa
na bifu na mimi binafsi simchukii msanii yeyote na sina bifu na yeyote.
Swali: Video yako ya Mwana imezungumziwa na mashabiki kuwa
haikuwa na uhalisia. Pia ilikuwa ya kawaida sana, wewe binafsi unalichukuliaje?
Ali Kiba: Video ilivyokuwa ndivyo ilipangwa iwe kwa sababu kila mtu alikuwa
amejenga picha itakuwaje kwa hiyo ililazimika kufanya vile kwa kuwa watu
walishapanga mpaka gharama kwa kuwa nilikaa muda mrefu pasipo kufanya.
Ningefanya
kitu ambacho watu walikifikiria kiukweli ingekuwa karaha, nilichozingatia mimi
ni kuimba vizuri na kuonyesha fikra za wimbo husika.
Swali: Vipi uliandaa ‘skripti’ ya video au aliamua GodFather
kuifanya vile ilivyotengenezwa?
Ali Kiba: Tulikuwa na ‘script’ yetu pia waongozaji wa video walikuwa na yao ambayo
walitupatia. Hivyo tukakubaliana nao kwa sababu tulitaka kuleta utofauti na
kila kitu kikakaa sawa.
Swali: Ni kweli kwamba una mpango wa kufanya kolabo na Chris
Brown?
Ali Kiba: Uwezekano wa kufanya upo kwa sababu kila kitu ni mipango kwa
hiyo naweza kufanya kolabo na wasanii wa kimataifa na mashabiki watarajie
kufanya hivyo.
Swali: Kwa nini haujafanya video ya Kimasomaso na ulisema
video ya Mwana ingefanyika Dar es Salaam kwa nini ulitengenezea Afrika Kusini?
Ali Kiba: Video ya ‘Kimasomaso’ ilishindikana kutokana na muda ulikuwa
hautoshi, nilijikuta niko katika mambo mengi sana kwani nilikuwa nimeegemea
katika video ya Mwana kwa hiyo nilipokuja kugeuka ikawa ni vigumu.
Nilisema kwamba nyingine ningefanya nje ya hapa lakini kwa
‘Mwana’ sijaelewa kwanini nifanye hapa, tofauti na hiyo nyimbo haikuwa na maana
ya Dar es Salaam, maana yake ni mwanamke na mwanamume sikuona sababu ya
kufanyia hapa jijini.
Ukitumia neno la Dar es Salaam ni kwa sababu ni jiji lenye changamoto kwa hiyo
unapozungumzia hilo ina maana kwamba ni Joharnesburg, Nairobi, Kampala, London
majiji ambayo yana changamoto mfano video ya Macmuga nilifanyia Marekani.
|
No comments:
Post a Comment