UJIRANI MWEMA:-Tazama Yaliyojiri jana februari 14,2015 wakati Chama cha CNDD-FDD cha Burundi kikifungua Ofisi yake wilayani Giteranyi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 15, 2015

UJIRANI MWEMA:-Tazama Yaliyojiri jana februari 14,2015 wakati Chama cha CNDD-FDD cha Burundi kikifungua Ofisi yake wilayani Giteranyi.

Ofunguzi wa Ofisi hiyo ya Chama Tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD iliyojengwa kwa nguvu ya Wanachama katika wilaya ya Giteranyi ,mkoa wa Muyinga nchini humo, hapo jana Februari 14,2015 Ulihudhuriwa na Ujumbe na Viongozi wa Chama Tawala cha Mapinduzi CCM - Nchini Tanzania kutoka wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

 Chama cha Mapinduzi CCM -Tanzania na Chama cha CNDD-FDD -Burundi vimekua na mahusiano mazuri hali inayopelekea kushirikiana katika mambo mbalimbali ya Kiharakati katika kukuza Demokrasia.


Kutoka kushoto ni MMNEC wilaya ya Ngara Bw.Issa Samma,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ngara Bw.Hadson Bagege katikati akiwa na Mkewe kushoto wakati wa Ofunguzi wa Ofisi hiyo ya Chama Tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD iliyojengwa kwa nguvu ya Wanachama katika wilaya ya Giteranyi ,mkoa wa Muyinga nchini humo.Picha Na:-Shaban Ndyamukama.





UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad