|
Mita za umeme....Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeliagiza Shirika la Umeme
nchini (Tanesco) kupunguza bei za umeme kuanzia Machi Mosi mwaka huu,2015.
Akitoa agizo
hilo jijini Dar es Salaam jana Februari 13,2015, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi
amesema kutokana na mabadiliko kwenye bei ya mafuta, thamani ya shilingi na
mfumuko wa bei, gharama za kununua umeme zinatakiwa zishuke kwa asilimia 2.21.
Akifafanua
amesema wateja wenye matumizi ya kawaida, bei ya umeme itashuka kutoka sh306
kwa uniti hadi sh298 kwa uniti sawa na punguzo la sh8 kwa uniti moja.
Amesema
mwananchi anayenunua umeme wa sh 10,000 anapata uniti 32.6 hivi sasa, lakini
baada ya punguzo hilo kwa fedha hiyo hiyo atapata uniti 33.5.
Marekebisho hayo
ni kwa bei ya kununua uniti ya umeme na si kwa tozo za mwezi za utoaji huduma.
“Wateja
wenye biashara ndogo ndogo ambao wapo kwenye kundi la T2 wao bei zitashuka kwa
sh5, wateja wa viwanda vya kati bei zitashuka kwa sh4, wateja wa viwanda
vikubwa na migodi likiwemo Shirika la Umeme Zanzibar wao bei itashuka chini kwa
sh3 kwa kila uniti moja,” amesema Ngamlagosi.
Hata hivyo,
amesema wateja wanaotumia umeme chini ya uniti 75 kwa mwezi ambao hununua uniti
moja kwa sh100 hawatanufaika na punguzo hilo kwa kuwa wanapata ruzuku kutoka
kwa wateja wakubwa.
|
No comments:
Post a Comment