|
Sehemu ya
Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo
pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Leo hii Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), imesogeza mbele zoezi hilo la uandikishaji
wa wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura hadi Februari 23, mwaka
huu 2015, huku vyama vya siasa vikilalamikia kutoshirikishwa na utendaji kazi
wa kusuasua wa Tume hiyo.
Mwenyekiti
wa Nec, Jaji Damian Lubuva, alitangaza hatua hiyo Februari 12,2015 wakati wa
mkutano wa pamoja baina ya vyama vya siasa na Nec kujadili zoezi hilo la
uandikishaji wa wapigakura katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura chini ya
mfumo wa Biometric Voter Registration (BVR).
Anasema
awali NEC ilipanga zoezi hilo lianze Februari 16, mwaka huu, lakini kutokana na
maoni ya wadau kutaka lisogezwe mbele, wameamua litaanza Februari 23, mwaka
huu, ili kutoa nafasi kwa vyama vya siasa kuweka mawakala katika vituo
mbalimbali vya uandikishaji.
Hata hivyo,
alipoulizwa zoezi hilo litaendelea hadi wakati gani, anasema kwa sasa ni vigumu
kueleza kwa kuwa vifaa (BVR kits) vilivyopo ni 250, na matarajio ni kupata
vifaa 7,750 ambavyo vitawezesha zoezi hilo kukamilika nchi nzima kwa muda
mfupi.
“Tumeongeza
muda wa wiki moja ili kutoa nafasi kwa vyama vya siasa kuweka mawakala na
kuelimisha wananchi umuhimu wa kujitokeza kuandikishwa…hatuna haja ya
maandamano njooni ofisini tutawasikiliza kama tulivyowasikiliza kwenye ombi la
kusogeza mbele muda,” alisema Jaji Lubuva.
Wakizungumza
katika mkutano huo, viongozi wa vyama vya siasa waliitaka NEC kuwa wazi na
kutoa taarifa kwa wakati na majibu mazito kwa maswali yanayoulizwa na siyo
kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu.
Pia viongozi
hao waliitaka Tume hiyo kuweka wazi ni kiasi gani cha fedha wamepata na
matumizi ya vyombo vya dola katika ulinzi wakati wa uandikishaji ambao utatisha
au majeshi yatatumiwa kwa malengo ya kisiasa.
|
No comments:
Post a Comment