Rais Jakaya
Kikwete akizindua rasmi Sera ya Elimu ya Taifa Dar es Salaam jana. Kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik.
Ubora.
Alisema sera
hiyo imezingatia stadi za msingi ambazo ni kuandika, kusoma na kuhesabu, ili
kuwezesha watoto kujengwa kwenye msingi mzuri na hata kwenye Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN) hilo limezingatiwa.
“Hata kwenye
mpango wa BRN tumelizungumza ili kuhakikisha inatolewa elimu bora.Tusifanye
mambo ya kuchekesha mtoto anafika madarasa ya juu hajui kuandika, kusoma na
kuhesabu. “Kuanzia sasa kama mtoto anafika darasa la pili, hajui kusoma,
kuandika na kuhesabu (KKK), ni bora asiende darasa la tatu…naamini watoto
wakiimarishwa katika stadi za KKK itaondoa matatizo haya,” alisema.
Tathimini ya
Msingi ya Taifa kwa ajili ya uwezo wa wanafunzi katika KKK, kwa wanafunzi wa
Darasa la Pili iliyofanyika mwaka jana, ilibaini kuwa asilimia 98 ya wanafunzi
wa Darasa la Pili nchini, walikuwa hawaelewi wanachokisoma.
Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema, tathimini hiyo
imefanywa kwa baraka za Wizara yake kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la
Marekani (USAID), ili kupata taarifa kuhusu hali halisi ilivyo ya wanafunzi wa
Tanzania kumudu stadi za KKK wanapofika Darasa la Pili.
Mafanikio.
Mbali na
mafanikio ya kufikia uwezo wa kuanza kutoa elimu ya msingi na sekondari bure,
huku msisitizo ukiwekwa katika utoaji wa elimu bora, Rais Kikwete pia
ilitangaza mafanikio mengine katika sekta ya elimu ambayo yamefikiwa katika
uongozi wake wa miaka kumi.
Rais Kikwete
alisema sasa elimu imepewa kipaumbele katika sera na shughuli za serikali, ndio
maana Bajeti ya Elimu, ndio kubwa kuliko bajeti zote.
Alifafanua
kuwa mwaka 2005/06 bajeti hiyo ilikuwa Sh bilioni 6.7, wakati mwaka huu wa
fedha imepanda na kufikia Sh trilioni 3.1.
Hatua hiyo
ya kibajeti kwa mujibu wa Rais Kikwete, ni ongezeko la mara tano ya Bajeti ya
mwaka 2005 sawa na asilimia 20 ya Bajeti ya Serikali ambayo inatengwa kwa ajili
ya elimu.
Katika suala
la mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema imetoka
Sh bilioni 56 kwa mwaka wa fedha 2005/06, hadi kufikia Sh bilioni 345 kwa mwaka
huu wa fedha.
Aidha, kwa
mwaka jana 2014, wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu, waliongezeka
kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000.
Kwa upande
wa shule za msingi, alisema zimeongezeka kutoka 14,000 kwa mwaka 2005 hadi
kufikia shule 16,343 kwa mwaka 2014, huku shule za sekondari zikiongezeka
kutoka 531 kwa mwaka 2005, hadi kufikia 4,576, mwaka 2014.
Idadi
wanafunzi wanaojiunga na sekondari, Rais Kikwete alisema imeongezeka kutoka wanafunzi
524,325 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi milioni 1.8.
Rais Kikwete
alisema pia vyuo vya ufundi vimeongezeka kutoka vyuo 184 mwaka 2005 na kufikia
vyuo 744 kwa mwaka 2014, huku vyuo vikuu vikiongezeka kutoka vyuo vikuu 26
mwaka 2005 na kufikia vyuo vikuu 50 kwa mwaka 2014.
Alikumbusha
kuwa kama sio kuanzishwa kwa shule za kata, idadi ya wanafunzi pia
isingeongezeka.
“Hali
imebadilika, sasa wanafunzi wengi wanakwenda shule na vyuoni na suala la watoto
na vijana kupata fursa ya kusoma, sio tatizo katika sekta ya elimu, sasa
kinachotakiwa ni kuhakikisha inapatikana elimu bora kwa kuboresha mazingira ya
elimu,” alisema Rais Kikwete.
Source:-Habari leo.
|
No comments:
Post a Comment