SOKA LETU ULAYA:-Picha na Matokeo ya mechi za leo Jumamosi Februari 07,2015 Arsenal,Real Madrid wakipoteza Pointi Muhimu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 07, 2015

SOKA LETU ULAYA:-Picha na Matokeo ya mechi za leo Jumamosi Februari 07,2015 Arsenal,Real Madrid wakipoteza Pointi Muhimu.

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015: -Mabingwa wa Watetezi wa Soka nchini Uingereza, Manchester City, Leo hii Februari 07,2015 wakiwa kwao Etihad wametoka Sare na Hull City na kuwaruhusu Vinara Chelsea kuongoza Ligi wakiwa Pointi 7 mbele yao baada ya kushinda Ugenini Bao 2-1 dhidi ya Aston Villa.

 Man City walinusurika kufungwa na Hull City walioongoza kwa Bao la Dakika ya 35 la David Meyler na kusawazisha Dakika ya 90 kwa Bao la James Milner.

Chelsea, wakicheza Ugenini Villa Park, walifunga Bao la Kwanza Dakika ya 8 kupitia Eden Hazard na Villa kurudisha Dakika ya 48 kupitia Jores Okore lakini ni Branislav Ivanovic, kwenye Dakika ya 66, ndie aliewapa ushindi kwa kufunga Bao safi kwa kigongo.

Nao  Tottenham Hotspur wakaifunga Arsenal Bao 2-1 baada ya kutoka nyuma kwa Bao 1 kwani  Arsenal walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 11 la Mesut Ozil ambalo lilidumu hadi Mapumziko kwenye mechi hiyo ya mapema leo hii Februari 07,2015.
Mchezaji  Harry Kane aliibuka Kipindi cha Pili na kupiga Bao 2 katika Dakika za 56 na 86.

Msimu huu Harry Kane ameshapiga Bao 22 na Leo ameifanya Tottenham waitambuke Arsenal na kukamata Nafasi ya 5 kwenye Ligi na Arsenal wako Nafasi ya 6 Pointi 1 nyuma yao.

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015- RATIBA.

**Saa za Bongo

Jumapili Februari 8,2015.

1500 Burnley v West Brom    
     
1705 Newcastle v Stoke  
           
1915 West Ham v Man United   
           
Jumanne Februari 10,2015.

2245 Arsenal v Leicester  
          
2245 Hull v Aston Villa   
            
2245 Sunderland v QPR  
           
2300 Liverpool v Tottenham  
              
Jumatano Februari 11,2015.

2245 Chelsea v Everton   
          
2245 Man United v Burnley   
               
2245 Southampton v West Ham 
          
2245 Stoke v Man City  
             
2300 Crystal Palace v Newcastle 
          
2300 West Brom v Swansea  

LA LIGA 2014/2015:-Vinara  wa Ligi hiyo huko nchini Hispania, Real Madrid Leo Februari 07,2015 majira ya jioni wamechapwa Bao 4-0 na Wapinzani wao wa Jadi Atletico Madrid kwenye Dabi ya Jiji la Madrid Uwanjani Vicente Calderon kwenye Mechi ya Ligi.

Licha ya kipigo hiki, Real Madrid bado wanaongoza Ligi hiyo wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Barcelona na Timu ya 3 Atletico Madrid ambao ndio Mabingwa Watetezi wa La Liga.

Lakini Real Madrid walicheza wakiwa na pengo kubwa kwa kuwakosa Pepe, James Rodriguez na Sergio Ramos, ambao ni Majeruhi, na pia Marcelo ambae amefungiwa Mechi 1 baada ya kuzoa Kadi za Njano 5.

Hadi Mapumziko Atletico Madrid walikuwa mbele kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Tiago Mendes Dakika ya 14 na Saul Niguez Dakika ya 18.

Atletico waliongeza Bao la 3 Dakika ya 67 kupitia Griezmann na Mario Mandzukic kuhitimisha kwa Bao la 4 katika Dakika ya 90.

LA LIGA 2014/2015  RATIBA/MATOKEO.

**Saa za Bongo

Jumatano Februari 4,2015.

Real Madrid CF 2 Sevilla FC 1

Ijumaa Februari 6,2015.

Deportivo La Coruna 2 SD Eibar 0

Jumamosi Februari 7,2015.

Atletico de Madrid 4 – 0 Real Madrid CF 

2000 Villarreal CF v Granada CF

2200 Levante v Malaga CF

0001 Real Sociedad v Celta de Vigo

Jumapili Februari 8,2015.

1400 Cordoba CF v UD Almeria

1900 Getafe CF v Sevilla FC

2100 RCD Espanyol v Valencia C.F

2300 Athletic Bilbao v Barcelona

LIGI KUU UJERUMANI 2014/2015:-Borussia Dortmund Leo hii Februari 07,2015 wamejichomoa toka mkiani mwa Bundesliga baada ya kuichapa Freiburg Bao 3-0 Ugenini.

Ushindi huu umeifanya Dortmund ipande hadi Nafasi ya 16 wakiwa Nafasi ya 3 toka mkiani.

Bao za Dortmund hii Leo zilifungwa na Marco Reus na mbili za Mchezaji kutoka Gabon Pierre‑Emerick Aubameyang.

Nao Mabingwa Watetezi na Vinara wa Bundesliga, Bayern Munich, baada ya kuanza kwa kusuasua kwenye Ligi kwa kuchapwa 4-1 na Wolfsburg na kutoka Sare 1-1 na Schalke, Leo hii wamezinduka na kushinda Ugenini walipoichapa Stuttgart Bao 2-0 kwa Bao za Arjen Robben na David Alaba.

Ushindi huu umewafanya Bayern waongoze Bundesliga wakiwa Pointi 8 mbele ya Wolfsburg ambao nao walishinda Bao 3-0 walipocheza na Hoffenheim.

BUNDESLIGA 2014/2015 RATIBA\MATOKEO.

**Saa za Bongo

Jumamosi Februari 07,2015.

Mainz 0 - 2 Hertha Berlin 

Wolfsburg 3 - 0 Hoffenheim 

Freiburg 0 - 3 Borussia Dortmund 

Stuttgart 0 - 2 Bayern Munich

FC Cologne 0 - 0 SC Padeborn 

Hamburger 2 - 1  Hannover 96


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad