AFCON 2015:-DR Congo Mshindi wa Tatu,Jumapili Nani kuwa Bingwa kati ya Ghana V/s Ivory Coast..?? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 07, 2015

AFCON 2015:-DR Congo Mshindi wa Tatu,Jumapili Nani kuwa Bingwa kati ya Ghana V/s Ivory Coast..??

DR Congo wamemshinda mwenyeji wa Fainali ya Mataifa ya Africa,AFCON 2015, Equatorial Guinea baada ya kumfunga kwa penati  4-2 kufuatia mechi hiyo ya kumtafuta mshindi wa tatu wa fainali hizo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Hapo kesho Jumapili februari 08,2015,saa Nne usiku  huko Bata Nchini Equatorial Guinea, Bingwa wa Mataifa ya Afrika atapatikana baada ya Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, kuchezwa kati ya Ghana na Ivory Coast.

Hii ni Mechi inayokutanisha Vigogo wa Afrika ambao wote wameshacheza Fainali 3 zilizopita za Kombe la Dunia.

Ghana wamewahi kutwaa Ubingwa wa Afrika mara 4 lakini mara ya mwisho ni Mwaka 1982 wakati Ivory Coast imetwaa mara moja tu Mwaka 1992 walipoitoa Ghana.

Ivory Coast wametinga Fainali hii ya AFCON 2015 kwa kuitwanga DR Congo Bao 3-1 na Ghana kuwatoa Wenyeji Equatorial Guinea kwa Bao 3-0kwenye Mechi iliyojaa vurugu za Washabiki na kusimamishwa kwa zaidi ya Dakika 30.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad