|
Aidha pia Mkuu wa Mkoa
wa Kagera ,amebainisha kuwa Serikali Mkoani Kagera, inatarajia kufanya
Oparesheni dhidi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo katika kata ya Kasulo
wilayani Ngara na kwamba ni hali ya kuchosha
kusikia habari za wizi wa mifugo katika kata hiyo mara kwa mara, hivyo ni
lazima hatua zichukuliwe ili kudhibiti vitendo hivyo.
Bw Mongela
ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya baadhi ya wakazi wa kijiji hicho,
waliodai kuwa kwa sasa wafugaji hawana amani kutokana na kukithiri kwa vitendo
vya wizi wa mifugo huku wahusika wakiwa hawachukuliwi hatua zozote.
Akitembelea
nyumba ya Masista wa Buhororo mjini Ngara, wakati akikagua miradi ya maji
katika ziara yake ya siku 2, amewaagiza watendaji katika Halmashauri ya wilaya
ya Ngara kuhakikisha wanapeleka huduma muhimu kwa wananchi muda wote badala ya
kusubiri ziara za viongozi.
Amesema mara
nyingi wananchi wamekuwa hawapati huduma muhimu ikiwemo maji lakini huduma hizo
hupatikana pale viongozi wa juu wanapofanya ziara katika maeneo husika.
|
No comments:
Post a Comment