PICHA / HABARI:-Yaliyojiri leo Februari 12,2015 wakati NEC ikitoa Tathimini ya Mfumo wa Uandikishaji BRV pamoja na Kuzungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 12, 2015

PICHA / HABARI:-Yaliyojiri leo Februari 12,2015 wakati NEC ikitoa Tathimini ya Mfumo wa Uandikishaji BRV pamoja na Kuzungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo Februari 12,2015 kwenye Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar es salaam.

 Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi, Prof. Amon Challigha.Picha na Emmanuel Massaka
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akichangia mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo Februari 12,2015 kwenye Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa NEC, Julias Malaba akiwasilisha mada.
Pichani juu na chini ni  Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar es salaam.
Pichani juu na chini ni  Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar es salaam.
Muonekano wa mkutano huo.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania ‘’NEC” imetoa tathimini ya zoezi la majaribio (Pilot) la Uboreshwaji wa Daftari la Kudumua la Wapigaji Kura katika majimbo ya Kawe, Dare s salaam, Kilombero Morogoro, pamoja na Milele mkoani Katavi, kwa ajili ya kutumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration –(BVR).

Akizungumza na wanahabari leo Februari 12,2015, katika Ukumbi wa Golden Tower uliopo Posta Jijini Da er salaam,Mkurugenzi wa Tume, Bw.Julias Maluba amesema kuwa maandalizi mengine waliyofanya ni pamoja na uhakiki wa vituo vya kuandikishia wapiga kura, katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa, hivyo tume imefanikiwa kuongeza vituo vingine vipya kutoka vituo 24,919 hadi vituo 36,109 vya sasa.

Aidha Malaba ametaja changamoto walizokutana nazo ni pamoja na ‘setting’ za mashine inayotumika katika zoezi hilo la uchukuaji wa alama za vidole, majina ya wenye alama ‘ ( mfano wa jina ng’ombe) na zinginezo.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad