HABARI / PICHA :-Taswira ilivyokuwa wakati Madereva wa daladala Misungwi wakiziba Barabara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 12, 2015

HABARI / PICHA :-Taswira ilivyokuwa wakati Madereva wa daladala Misungwi wakiziba Barabara.

Baadhi ya magari yaliyoathiriwa na mgomo huo.

 Madereva wa daladala wilayani Misungwi, mkoani Mwanza wamefunga barabara kuu ya kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam wakitaka Serikali ya Wilaya Misungwi iwaoneshe vituo halali vya kuchukua na kushusha abiria.

Tukio hilo limetokea leo Februari 12,2015, majira ya saa sita mchana ambapo abiria wa Misungwi hawakuweza kwenda Mwanza Mjini sababu daladala zote ziligoma kwenda na kusababisha usumbufu kwa abiria waliokuwa wakisafiri kwa muda huo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi lilizima zoezi hilo kwa kuwatawanya watu hao kwa kuwa hawakufata taratibu za kisheria katika mgomo huo.

(PICHA/HABARI: Mashaka Kisusi, Mwanza.)

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad