Matatizo
katika uzalishaji wa mbegu za kiume inahusiana na kutokuwepo kwa mbegu za kiume
kwenye manii au uwepo wa mbegu kidogo sana katika manii.
Mbegu za
kiume huwa zinachunguzwa kwa kutumia kifaa maalum au darubini katika maabara,
kwa kawaida mwanaume ili aweze kumpa mwanamke mimba anatakiwa atoe kiasi cha
mbegu kati ya milioni ishirini hadi milioni mia tatu hamsini kwa tendo, chini
ya milioni ishirini huwezi kumpa mimba mwanamke.
Endapo
kiwango cha mbegu zitakuwa kidogo kitaalam hali hiyo huitwa ‘Oligospermia’ na
kama huna kabisa mbegu hali hiyo huitwa ‘Azoospermia.Dalili za kutokuwa na
mbegu za kiume
Hakuna
dalili za moja kwa moja kusema kwamba utaumwa kitu fulani, lakini dalili
zifuatazo huambatana na tatizo hili; kwanza ni kukaa katika mahusiano kwa
kipindi kisichopungua mwaka mmoja lakini mwenzi wako hapati mimba,
kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa uume kukosa nguvu’ Low sex Drive’ na
ukisimama unashindwa kuendelea na kumalizia tendo ‘Erectile dysfunction’ pamoja
na kuwahi kumaliza tendo la ndoa.
Maumivu na
uvimbe wa korodani, kupungua kwa vinyweleo na ndevu kutoota pia ni dalili
inayoashiria matatizo ya uzazi kwa mwanaume kwani ni ishara ya upungufu wa
Kromozomu au homoni za kiume.
Hizo zote ni dalili kuu za matatizo ya uzazi kwa mwanaume.
Wakati gani
wa kumuona daktari?
Endapo umekaa na mwenzio mwaka mmoja au zaidi, mnafanya tendo la ndoa bila
kinga yaani kizuizi chochote wakati wa kupangilia ujauzito lakini mimba
haipatikani.
Kama una matatizo ya nguvu za kiume au unawahi kumaliza tendo la
ndoa. Unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa au uume unalegea wakati wa tendo
pia ni mojawapo ya chanzo.
Unakuwa na
maumivu ya korodani au korodani kuvimba, maumivu ya uume na maumivu wakati wa
kukojoa au uwepo wa kivimbe katika uume.
Chanzo cha
tatizo
Uzalishaji wa mbegu za kiume unafuatana na ubora wa korodani kama haina tatizo
lolote na kiwango bora cha mfumo wa homoni mwilini mwake. Homoni zinadhibitiwa
katika ubongo na kuimarisha korodani zizalishe mbegu.
Mbegu zikishazalishwa,
husafirishwa na mirija midogo sana na laini hadi katika tezi dume’Prostate
gland’ ambayo kazi yake kubwa ni kuzalisha manii.
Matatizo
katika mbengu za kiume ni kutokuwepo kwa mbengu kunakosababishwa na hitilafu kwenye
korodani, kuzalisha mbegu zenye kasoro, mbegu zisizo na kiasi na mbegu chache.
Matatizo ya korodani husababishwa na joto kali katika korodani, maambukizi
katika korodani na uume na kuumia korodani.
Mishipa ya
damu kulalia korodani ‘Variocele’ pia ni mojawapo ya tatizo kubwa la kuziba kwa
mirija ya usafirishaji mbegu hizo.
Zipo pia
sababu za kimazingira zinazoathiri uzalishaji wa mbegu za kiume mfano kemikali
za viwandani, rangi za viwandani au majumbani, dawa za mashambani na za kuua
wadudu, mionzi ya X- Ray, kukaa kwenye joto kali, kuvaa nguo za kubana na
kukaa mahali kwa muda mrefu, kupakata kompyuta ‘Lap top’ kwa muda mrefu,
matumizi ya sigara, bangi na madawa mengine ya kulevya kwa muda mrefu na ulevi
uliokithiri. Uzito mkubwa wa mwili na matatizo ya akili.
Uchunguzi.
Uchunguzi wa tatizo hili hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya
kwa madaktari wa masuala ya uzazi.
Vipimo vya damu kuangalia mwenendo wa mfumo wa homoni mwilini Kipimo cha Ultrasound
kuangalia korodani yako kwa ndani.
Uchunguzi
hufanyika kisayansi hospitali tu, hakuna vifaa vingine vya kuchunguza kwa
kubahatisha, unatakiwa utolewe damu, na utoe mbengu zako za kiume baada ya
kupumzika kufanya tendo la ndoa angalau kwa siku tatu.
Matibabu na
ushauri.
Hufanyika baada ya uchunguzi ambapo daktari atatoa dawa kuzingatia na tatizo
lililopo.
Kama hakuna mbegu zipo chache au kuna maumivu au kasoro zozote.Uwepo wa
kasoro za viungo vya uzazi pia ni tatizo mfano, uume mfupi, kutokuwa na korodani
au kuwa na korodani moja. Wahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.
Source:
Global Publisher
|
No comments:
Post a Comment