Ghana 3-0 Equatorial Guinea AFCON 2015:-Fainali Februari 08,2015 na Ivory Coast ambayo haijawahi kuwa Bingwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 06, 2015

Ghana 3-0 Equatorial Guinea AFCON 2015:-Fainali Februari 08,2015 na Ivory Coast ambayo haijawahi kuwa Bingwa.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ghana wakishangilia ushindi wao baada ya kuwaondosha wenyeji wa fainali za kombe la mataifa kwa mwaka huu AFCON 2015,a Equatorial Guinea na kuwaondoa katika ndoto ya kutwaa ubingwa wa kombe  la mataifa ya Africa, baada ya kufungwa mabao 3-0 Mjini Malabo.

 Lakini aibu kubwa imetawala baada ya mashabiki wa timu mwenyeji kufanya vurugu kubwa katika uwanja wa Malabo jana Februari 05,2015 usiku na kusababisha mechi kusimama kwa dakika 35.




Bao za Ghana zilifungwa na Penati ya Jordan Ayew Dakika ya 42, Wakaso Dakika ya 45, na Andre Ayew Dakika ya 75.

Wenyeji wameonesha kiwango kikubwa na maajabu makubwa katika michuano ya mwaka huu, lakini kutolewa hatua ya nusu fainali kuliwaudhi mashabiki ambao walirusha chupa kwa wachezaji wa Ghana, viongozi na mashabiki.

Ghana, ambao washawahi kuwa Mabingwa wa Afrika mara 4 ingawa hawajatwaa Ubingwa huo tangu 1982, wanatinga Fainali kucheza na Ivory Coast ambayo haijawahi kuwa Bingwa ingawa safari hii imesheheni Mastaa kibao wanaocheza Ulaya.



Jumatano ya februari 04,2015 Usiku , kwenye Nusu Fainali ya kwanza, Ivory Coast iliichapa Congo DR Bao 3-1.

Fainali itachezwa Jumapili Februari 08,2015 ndani ya Estadio de Bata, Mjini Bata.

  MSHINDI WA TATU

Jumamosi Februari 07,2015.

2100 Congo DR v Equatorial Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]   
  
FAINALI AFCON 2015.

Jumapili Februari 08,2015.

2200 Ivory Coast v Ghana [Estadio de Bata]     

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad