|
Wasifu wa marehemu ukisomwa.
Na
Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma
KAMANDA wa
Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME –
SACP amesema kama alivyotoa taarifa juzi tarehe 04/02/2015 kuhusiana na kuawa
kwa Askari Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI huko Chang’ombe ya juu
mkoani Dodoma na mtu aliyefahamika kwa jina la TISSI S/O SIRIL MALYA.
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya
kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga kichwani na
mikononi askari huyo.
Kamanda
MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti
Mkavu Mailimbili mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua
askari.
Hata hivyo
walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake,
Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa
lakini daktari akagundua ameshafariki.
Aidha
Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba
mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka
2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua.
Ametoa
pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea askari
wetu lakini waache kujichukulia sheria mkononi.
Pia ametoa
wito kwa wananchi waanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya
familia kwani imeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba
ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.
|
No comments:
Post a Comment