AJALI:-Picha Jinsi basi la Adventure likipinduka baada ya Kugongwa na Lori la Mchanga Leo Februari 24,2015 wilayani Kibondo na Watu 60 Kunusurika Maisha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 24, 2015

AJALI:-Picha Jinsi basi la Adventure likipinduka baada ya Kugongwa na Lori la Mchanga Leo Februari 24,2015 wilayani Kibondo na Watu 60 Kunusurika Maisha.

Watu Zaidi ya 60 wamenusurika kupoteza Maisha wilayani Kibondo mkoani Kigoma  baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kwenda mkoani Kigoma,kupinduka baada ya kugongwa na gari la mchanga lililoingia barabara kuu gafla,kutokana na kufeli mfumo wake wa breki.

 Radio Kwizera imeshuhudia Basi hilo la kampuni ya Adventure lenye namba za usajiri T 133 AGD ( Pichani ) likiwa limepinduka majira ya saa nane mchana huku abiria Zaidi ya 60 wakiwa wanaokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa kutumia magari ya halmashauri ya wilaya ya Kibondo.

Baadhi ya mashuhuda wamesema kuwa gari aina ya Lori tipa lenye namba za usajiri T 420 CPQ lilifeli mfumo wa break na lilikuwa likiteremka kuingia barabara kuu ndipo likagongana na basi kisha kugeuka na kuangalia liliko toka huku basi likipinduka baada ya kugonga ukingo wa barabara

Source:-Radio Kwizera.

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad