AJALI:-Picha / Habari Ni kuhusu Basi kugongana uso kwa uso na Lori na kuua Watu wawili Papo Hapo Dodoma leo Februari 19,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 19, 2015

AJALI:-Picha / Habari Ni kuhusu Basi kugongana uso kwa uso na Lori na kuua Watu wawili Papo Hapo Dodoma leo Februari 19,2015.

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya KIDIA ONE lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza kugongana uso kwa uso na lori la mizigo ( Pichani )lililokuwa likitoka Dodoma kwuelekea Morogoro katika kijiji cha vikonje kata ya mtumba nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Februari 19,2015 Majira ya saa Saba Mchana.

Katika eneo la ajali ambapo mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo dereva msaidizi wa basi aliyejitambulisha kwa jina moja la Makubeli akisema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya basi kuharibika mfumo wa breki na kumshinda dereva mwenzake kauli inayopingana na mmoja kati ya abiria aliyekuwemo kwenye basi hilo ambaye anadai chanzo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita basi jingine lililokuwa mbele yao bila tahadhari na ghafla akakutana uso kwa uso na lori.


Picha zote Na:Mwanawamakonda WhatsApp .....UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema ajali hiyo imehusisha Basi lenye namba za usajili T. 663 AXL aina ya SCANIA Kampuni ya KIDIA ONE lililokuwa litokea Dar es Salaam kwenda Mwanza likiendeshwa na ADAM s/o ROBERT, 38yrs, kabila Mnyaturu, mkazi wa Tegeta Dar es Salaam, liligongana uso kwa uso na Lori namba T.469 CFG Scania lenye Tellar T. 756 AZX.

Kamanda MISIME amewataja waliofariki dunia kuwa ni FADHILI S/O HAMIDU SAIDI miaka 36, Kabila Msukuma ambaye ni dereva wa Lori na utingo wa Bus aliyehafamika kwa jina la CHOGO S/O CHIGUNDA, miaka 30, Kabila Muha wote wakazi wa Dar es Salaam.

Majeruhi katika ajali hiyo ni 45 kati yao 34 ni wanaume na 11 ni wanawake; wengine wametibiwa na kuruhusiwa. Waliolazwa ni 24 kati yao wanaume ni 17 na wanawake ni 7.

Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali ni dereva wa Bus Kushindwa kuchukua tahadhali wakati wa kulipita gari lingine “over take”, na kusababisha ajali hiyo.

Aidha Kamanda  MISIME ametoa wito kwa madereva kuwa na udereva wenye tahadhali na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kwani dereva huyu wa basi angezingatia hilo ajali hii haingetokea na hatakama ingetokea madhara yake hayangekua makubwa kiasi hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad