AFCON 2015:-Equitorial Guinea yaibamiza Tunisia Lakini Mwamuzi wa mchezo Akipata cha Moto…Tazama Picha Hapa.’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 01, 2015

AFCON 2015:-Equitorial Guinea yaibamiza Tunisia Lakini Mwamuzi wa mchezo Akipata cha Moto…Tazama Picha Hapa.’’

Polisi na walinzi wa uwanjani hapo walilazimika kufanya kazi ya ziada kumuokoa Mwamuzi wa mchezo huo kati ya wenyeji Equatorial Guinea dhidi ya vigogo Tunisia  Rajindraparsad Seechurn pichani.



Wenyeji Equatorial Guinea wameshinda Mechi yao ya Robo Fainali za AFCON 2015, Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Tunisia Bao 2-1 kwenye Mechi iliyokwenda Dakika 120 za Mchezo huko Estadio de Bata Mjini Bata hapo Jana Januari 31,2015,usiku.

Equatorial Guinea sasa wapo Nusu Fainali na watacheza na Mshindi kati ya Ghana na Guinea.

Hii Leo Frebruari 01,2015, Robo Fainali zitakamilika kwa Ghana na Guinea kucheza huko Estadio de Mongomo Mjini Mongomo na kufuatiwa na Ivory Coast na Algeria huko Nuevo Estadio de Malabo Mjini Malabo.

Lakini Mwamuzi wa mchezo huo kati ya wenyeji Equatorial Guinea dhidi ya vigogo Tunisia Rajindraparsad Seechurn aliishia kukimbizwa na wachezaji wa Tunisia wakitaka kumdunda.


Wachezaji hao walihisii mwamuzi huyo alitoa penalti kwa wenyeji na haikuwa penalti na wenyeji hao wakafunga na kusababisha mechi iongezwe dakika 30 na mwisho wakaishia kushinda 2-1 na kuwatoa Tunisia.

Mara baada ya mechi, mwamuzi huyo alikuwa katika wakati mgumu huku wachezaji wa Tunisia wenye jazba kama nyati wakimkimbiza.


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad