|
TAARIFA
MUHIMU KABLA YA KUTUMIA PENICILLIN.
Mgonjwa,
unatakiwa kumuuliza daktari au mfamasi juu ya madhara yanayoweza kutokea
pale utakapo anza kutumia dawa hii. Baadhi ya madhara haya yanachukua muda
mrefu kama ambavyo nitaeleza baadae.
Baadhi ya dawa
za tiba huwa zina madhara kama zitumika sambamba na dawa nyingine. Kama
unatumia dawa za kupanga uzazi mweleze daktari, mfamasi au muuguzi.
Baadhi ya
dawa pia zinaweza kumdhuru mtoto aliyetumboni au anayenyonyeshwa kama
zitatumiwa na mjamzito au anayepanga kuwa mjamzito.
Pia mweleze
dakatri au mfamasia au muuguzi kama huwa unapata mzio unapotumia baadhi ya dawa
za tiba au unatia dawa za tiba kwa wakati huo au matatizo mengine ya kiafya.
Ni vyema pia
kutoa taarifa daktari au mfamasi au muuguzi kabla ya kutumia penicillin kama
una matatizo mengine ya kiafya kama vile magonjwa ya figo, ugonjwa unaoharibu
seli za chembe chembe nyeupe (mononucleosis), kutokwa na damu mwilini, na
tumbo/utumbo.
MATUMIZI
SAHIHI YA PENICILLIN.
Tumia dawa
ya penicillin kwa kunywa na maji kabla ya kula. Kunywa dawa hii kwa glasi nane
za maji.
Muulize
dakatari juu ya ukubwa wa glasi ya maji. Pia baadhi ya dawa katika kundi hili
zinaweza wakati umekula. Muulize dakatri au mfamasia au muuguzi namna bora
kutumia dawa hizi.Kama unatumia Pencillin G, unashauriwa kutotumia juisi ya
matunda yenye tindikali kama vile machungwa na vinywaji vingine vya jamii
hii mpaka ipite saa moja mara baada ya kutumia dawa.
Ili dawa hii iweze
kukusaidia unatakiwa kutumia kwa kiwango na wakati uliolekezwa kutumia. Hupaswa
kuacha kutumia dawa pasipo ruhusa ya daktari hata kama unahisi kupata nafuu au
kupona.
Kama utasahu
kutumia Penicillin, tumia pindi unapokumbuka. Kama muda uliokumbuka unakaribia
ule unaofuata, acha kutumia dawa, subiri muda unaofuata ufike ndipo utumie, na
kisha uendelee na utaratibu wa kawaida. Usikariri dawa.
Usigawe dawa
zako kwa mgonjwa mwinge au kutibu magonjwa mengine. Unatakiwa kuweka dawa mbali
na watoto na hupaswi kutumia dawa zako na mtu mwingine.
Hakikisha dawa
unayotumia haijaisha mmuda wa matumizi. Kama itakulazimu kununua dawa, basi
nunua kutoka katika duka linalotambuliwa na Serikali.
Duka la dawa
linalotambuliwa na serikali ni lile lilisajiliwa na Baraza la Famasi na utaitambua
kwa kuangalia cheti kilichotundikwa dukani.
|
No comments:
Post a Comment