Gari jipya aina ya Nissan Murano la staa wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake,
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Stori: GPL.
Lile gari jipya aina ya Nissan Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Beautiful Onyinye,
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limezua mapya ambapo baada ya kudai linamchefua sasa
anadaiwa kuwa analiuza kwa kigezo kwamba hataki gundu mwaka huu mpya wa 2015.
KUMBE
LIPO KWA DALALI
Habari za kiwango kutoka kwa mnyetishaji wetu zilidai kwamba gari hilo lipo kwa
dalali wa kike maarufu ajulikanaye kwa jina moja la Tindwa kwa ajili ya
kulitafutia mteja.
NI
KISASI?
Ilidaiwa kwamba, Wema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa ana kisasi na hasira kwa
Diamond kwa kuwa jamaa huyo kwa sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na staa wa
Uganda, Zarinah Hassani ‘Zari au The Boss Lady’.
“Watu
wanadhani Wema anafurahishwa na Diamond kutupia mapicha na Zari baada ya
kuwasifia juzikati.
“Ukweli ni kwamba hivi sasa Wema anakereka sana na jinsi Diamond anavyoweka
mapicha yake na Zari wakiwa sehemu mbalimbali na anaona kuwa na gari
ambalo amepewa zawadi na Diamond ni kujipa kero zisizokuwa na sababu
hivyo ameamua kuliuza,” kilisema chanzo hicho.
|
No comments:
Post a Comment