WAZIRI MPYA NISHATI NA MADINI:-Simbachawene asema Watanzania wamuamini katika kuwafikishia Maendeleo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 26, 2015

WAZIRI MPYA NISHATI NA MADINI:-Simbachawene asema Watanzania wamuamini katika kuwafikishia Maendeleo.

Waziri wa Nishati na Madini ,Bw.George Simbachawene amesema kuwa watanzania wamuamini ataendeleza kwa kasi ile ile katika kuwafikishia wananchi maendeleo kupitia sekta za nishati na madini.
Hayo ameyasema leo Januari 26,2015,wakati alipoanza kazi rasmi katika Wizara hiyo akichukua nafasi ya Profesa Sospeter Muhogo aliyejiuzulu wiki iliyopita,amesema kila mtu sio mkamilifu hata mitume watu wengine hawakumuamini.

Bw.Simbachawene amesema ana uzoefu wa kufanya kazi na kuachana na vyeti kwani vyeti ni ziada lakini kalama ya uongozi ndiyo inayohitajika.

Aidha amesema wanaotilia shaka uteuzi wake watakuwa na kigezo lakini kila mtu hawezi kuamini kila binadamu ana mapungufu kwa namna anavyoona mtu.

Simbachawene amesema atafuatilia usiri wa mikataba lakini sasa anasoma mazingira kwanza na kuweza kuweka bayana suala hilo.

Niko hapa watu waniamini kutokana na kazi zangu na watanzania waniamini niweze kufanya kazi niliyoaminiwa kwa niaba ya watanzania wenzangu”amesema Simbachawene.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Bw. Charles Mwijage akizungumza na waandishi wa habari mada baada ya kuwasili Wizarani hapo mapema leo januari 26,2015, asubuhi

Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini,Bw. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo Januari 26,2015
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad