TAZAMA PICHA/HABARI:-Juu ya Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw Amantius Msole wilayani Ngara mkoani Kagera leo Januari 26,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 26, 2015

TAZAMA PICHA/HABARI:-Juu ya Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw Amantius Msole wilayani Ngara mkoani Kagera leo Januari 26,2015.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw Amantius Msole kulia leo Januari 26,2015,amefanya ziara Wilayani Ngara mkoani Kagera ya kutembelea Vituo vya Forodha mkoani Kagera na alipokutana na wadau wa Maendeleo  hapa wilayani ,ametoa wito kwa watanzania waishio mipakani kutumia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na vituo vya forodha katika  mipaka ya kimataifa  kujikwamua kiuchumi katika  Jumuia ya Afrika ya Mashariki.

 

Amesema Soko la pamoja linatoa fursa ya kutafuta na kununua au kuuza bidhaa  na kuweza kubaini bei inayotosheleza mahitaji na kuongeza  uzalishaji mali  wa bidhaa  zinazopatikana kila nchi Mwananchama .  

Hata hivyo amesema jamii inahitaji  kuelimishwa fursa zilizowazunguka  ili kukuza uzalishaji  mali wenye tija wenye  kuinua kipato cha mwananchi anapozalisha  mazao na bidhaa mbalimbali  na kuboresha maisha yao.

Bw Msole amebainisha kuwa,'' Kwa upande wa biashara kuna uhuru wa kuongeza mitaji bila kuzuiliwa kwa kuonesha paspoti kwani lengo la soko la pamoja na kupanua  uwekezaji ambapo mfumo wa kifedha umewekwa pande zote katika nchi Wananchama..';

Pichani ni Naibu katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw Amantius Msole akitazama maendeleo ya ujenzi wa kituo cha forodha cha Kabanga kinachounganisha mpaka wa Nchi ya Tanzania na Burundi wakati wa ziara yake leo Januari 26,2015, Wilayani Ngara mkoani Kagera ya kutembelea Vituo vya Forodha mkoani Kagera.




Naibu katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw Amantius Msole akibeba udongo wakati alipotembelea kujionea  maendeleo ya ujenzi wa kituo cha forodha cha Kabanga kinachounganisha mpaka wa Nchi ya Tanzania na Burundi wakati wa ziara yake leo Januari 26,2015.


Naibu katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw Amantius Msole kulia akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ofisi ya wilaya ya Ngara ,kushoto kwake ni Kaimu mkurugenzi wa  idara ya Biashara na uzalishaji wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr Abdullah Makame.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw Amantius Msole kushoto akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa Forodha katika Ofisi za Kobero nchini Burundi .

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad