|
TAKUKURU
YASISITIZA KUCHUKUA HATUA
Wakati huo huo, Takukuru, imesisitiza kuwa wahusika waliomwaga pesa za Escrow
kwa watu mbalimbali wasubiri mtikisiko hatua za kisheria.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Takukuru, Dk. Edward Oseah,
alisema wananchi wategemea kuona mkono wa dola ukiwashukia wahusika
wakati wowote kuanzia sasa.
Alikuwa akizungumzia hatua za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa Escrow
wakiwamo viongozi na watendaji wa serikali na taasisi zake.
Akizungumza kwa methali, Dk, Oseah, alisema kinachofanyika ni kuondoa
matawi ya mti na kitakachofuatia muda mfupi ni kuchimbua na kung’oa
mizizi.
“Nawaomba wananchi wavute subira, kinachofanyika hivi sawa sawa na kuondoa
matawi ya mti wenye matatizo, lakini huwezi kuondoa matawi peke yake
lazima uchimbue na mizizi yote,” alisema Dk. Oseah.
Alisema anajua wananchi wanataka kuona hatua hiyo inakwenda mbali na kuwafikia
wale waliohusika waliotoa pesa hizo, lakini lazima utaratibu wa kisheria
ufuatwe.
“Haya ni mambo ya kisheria, lazima kufuata utaratibu ninachosema watuache
tufanye kazi, hakuna atakayeachwa katika jambo hili,” aliongeza kusema.
Pamoja na maofisa waliopandishwa kizimbani jana wengine waliowatangulia ni
Mhandisi mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijni (Rea) Theophilo John Bwakea na
Mkurugenzi idara ya Fedha, Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi Rugonzibwa
Theophil Mujunangoma ambao wanakabiliwa na mashitaka ya kupokea rushwa kutoka
kwa James Buchard Rugemalira.
Bwakea alidaiwa kuwa February 12 mwaka 2014, alipokea Shilingi milioni 161.7,
kutoka kwa Rugemalira ambayo ni sehemu ya fedha za akaunti ya Tegeta
Escrow kupitia akaunti yake iliyoko Mkombozi.
Aidha, Mujunangoma alidaiwa kuwa February 5, mwaka jana alipokea rushwa
ya Shilingi milioni 323.4 kutoka kwa Rugemarila.
Chanzo:-
NIPASHE
|
No comments:
Post a Comment