UHALIFU:- Mtuhumiwa Sugu wa ujambazi katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga na Simiyu atiwa mbaroni…Tazama Picha zaidi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 18, 2015

UHALIFU:- Mtuhumiwa Sugu wa ujambazi katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga na Simiyu atiwa mbaroni…Tazama Picha zaidi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP Valentino Mlowola akiwa na makamanda wenzake SACP Charles Mkumbo (Shinyanga) na  SACP Justus Kamugisha (Simiyu) wakati wakizungumza na waandishi wa habari kufuatia kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa wa ujambazi ambaye pia ni mfanyabiashara aitwaye Njile Samweli (46) marufu kwa “John” wa mjini Bariadi mkoani Simiyu, aliyekuwa akifanya matukio ya uhalifu katika Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida na Tabora.


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SCP Charles Mkumbo akionesha nguo ambazo zilikutwa kwa Mtuhumiwa kiongozi huyo wa genge la uhalifu ambazo zinasemekana ni za baadhi ya watu waliouawa wakiwemo majambazi aliokuwa akishirikiana nao ambao aliwauwa kwa maslahi yake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,SACP Charles Mkumbo akionesha silaha iliyokuwa ikitumiwa katika harakati za matukio ya ujambazi katika kijiji cha Idukilo Kata ya Luhumbo Mwadui wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga.Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,SACP Valentino Mlowola na kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,SACP Justus Kamugisha.

 
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad