UCHAGUZI JIMBO LA NGARA:-Wasome wanaozungumzwa Kuwania Jimbo hilo Mwaka huu 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 27, 2015

UCHAGUZI JIMBO LA NGARA:-Wasome wanaozungumzwa Kuwania Jimbo hilo Mwaka huu 2015.

Mbunge wa sasa,Ndugu Deogratius  Ntukamazima ambaye amesema kwamba hata gombea tena Ubunge wa jimbo la Ngara akihitaji kupumzika kutokana na kulitumikia taifa kwa muda mrefu.

  Homa ya Uchaguzi mkuu Nchi Tanzania mwezi October 2015,imetanda nchi nzima na hii inatokana na kwamba imebaki miezi michache kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani.

Uchaguzi huu unafanyika ukiwa umetanguliwa na ule wa Serikali za mitaa ambao kwa sehemu kubwa unatoa utabili wa majibu ya uchaguzi wa Ubunge na Udiwani kwenye majimbo yetu.

Leo nimeona ni vema nitumie haki yangu ya kikatiba ambayo kimsingi ni haki ya watanzania wote,haki ya kutoa maoni bila kuvunja sheria, natumia fursa ya haki hii ya msingi kutoa maoni yangu ya kiuchambuzi dhidi ya wagombea wanaotajwa na watu wengi kuwa na nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Ngara mkoani Kagera.

…..’’Wanaotajwa wako wengi lakini leo nitawazungumzia watano ambao kwa maoni yangu ndio wenye nafasi na ushawishi mkubwa kwa wananchi na vyama vyao.

Wagombea hao ni Ndugu Alex Gashaza,Mwalimu Gerald Muhile,Ndugu Rugumyamiheto,Mrs Herena Adrian kutoka CCM na Dr Petter Bujari wa chama cha CHADEMA.

Wagomba wote hao wanaingia au wataingia kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu 2015 kutaka kuirithi nafasi inayoachwa wazi kwa mujibu wa sheria na utashi wake,Mbunge Ndugu Deogratius  Ntukamazima .

Changamoto kubwa kwao itakua ni kuvaa viatu vya Mbunge huyu anaemaliza muda wake nasema anae maliza muda wake kwa sababu kwa sheria zetu ubunge hauna ukomo au kwa lugha nyingine ubunge hauna kustaafu ikiwa bado unakibali kwa wananchi au utashi wa kuendelea hiyo ni kwa mujibu wa sheria za Tanzania,..’’ 

Wanachangamoto kubwa ya kuvaa viatu vyake kwa sababu wakati unamuonesha Ntukamazima kuwa mbunge aliyefanya mengi kwa jimbo la Ngara na mambo hayo yako wazi mfano ni katika kipindi chake mradi wa maji vijijini umetekelezwa kwa ufanisi mkubwa, mradi wa scheme ya kilimo cha umwagiliaji umetekelezwa na pia mradi wa umeme vijijini umefanikiwa kwenye jimbo la ngara na kwa mujibu wa maelezo yake mradi wa barabara ya Lami Munzani -Burundi -Rulenge Ngara pesa zimeisha patikana hili ni deni kubwa kwa mbunge ajaye.

Huko nitoke nirudi kwenye mada kuu ya mgombea tarajiwa na nafasi yake kwa jamii.
 
NDUGU ALEX GASHAZA.

:- Huyu ni mwanasiasa mkongwe kabisa kwenye siasa za Ngara, ukimtoa Mama Herena kwa ukongwe hakuna mfano wake anazijua siasa za Ngara vizuri kuanzia upinzani mpaka za chama tawala hiyo kwake ni karata ya turufu lakini pia ni kipenzi cha watu wa pande zote mbili bughufi na bushubi kwa wanaofuatilia siasa za ngara wananielewa vizuri lakini pia Gashaza ana sifa ya mkazi mzawa ambayo amini usiamini ni karata yenye nguvu kubwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu 2015 kwenye jimbo la Ngara.

Gashaza amekua mkandarasi wa barabara na majengo kwa muda mrefu na hiyo ni taaluma yake na hilo laweza kumjenga au kumbomoa,kumjenga kwa sababu mbili kubwa moja limemkutanisha na watu wengi pande zote za wilaya na kujenga mahusiano na kupanua wigo wa kufahamika.

:-Piili ikiwa miradi aliyofanya aliitekeleza vizuri na manisha kwa kiwango na hakudhurumu mafundi na vibarua jambo hilo kwake ni mtaji.

:-Litambomoa likiwa mahali alipopita hakujenga mahusiano na watu na pili ikiwa hakuwapa ujira stahiki wale waliostahili kulipwa,kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa Gashaza ni mkongwe kwenye siasa za Ngara, hofu yangu ni je Chama(CCM) kinamkubali kama wananchi wanavyomkubali ..??

Nachelea kusema ikiwa hakubaliki kwenye chama, nafasi yake ya kusimamishwa kama mgombea inabaki shakani hata kama atashinda kwenye kura za maoni, kwa maoni yangu nikiulizwa ni mgombea mwenye nguvu lakini asiye kuwa na milango wazi serikalini, namanisha sio maarufu ngazi ya serikali na kichama kitaifa japo hoja hiyo sio tatizo kwa wapiga kura wa kawaida.

NDUGU RUGUMYAMIHETO
 
:-Huyu ni mtendaji mkongwe wa serikali na napata tabu kumuita mwanasiasa mkongwe kwa sababu sheria na taratibu zetu zinawakataza watumishi wa umma kuwa wanasiasa na kwa sababu hiyo kuwanyima fursa ya kuitwa wakongwe lakini itoshe kusema kwamba nafasi yake ya Ukatibu ilimpa uzoefu kwani ilimkutanisha na wanasiasa wengi wa nchi hii.

Rugumyamiheto itakua ni mara yake ya pili kugombea kama kumbukumbu zangu zitakua sahihi, hili nalo angarabu linampa kuzijua vizuri siasa za Ngara.

Uzoefu wake serikalini pia ni nafasi ya dhahabu kwake kusimamishwa na chama chake kwani uzoefu huo unaiacha milango mingi serikalini ikiwa haina kiburi cha kufunguka mbele yake ,kikwazo kikubwa kwa Rugumyamiheto ni Je anaubavu wa kuvuka mto na kuchukua kura ukiachilia mbali uhakika wa kuchukua kura za bugufi lakini pia utendaji wake kama katibu mkuu unamfungulia milango ngazi ya kitaifa? je? unamfungulia milango jimboni? anamaswali ya kujibu aliifanyia nini Ngara kwa nafasi ya baraka aliyokuwa nayo.

Kikwazo kingine cha wazi ni kikwazo cha ukazi kwa siasa za mwaka huu 2015 ,hilo swali hatalikwepa na hakuna mwanasiasa yeyote anayelitaka jimbo hili mwenye ubavu wa kuikwepa hoja ya ukazi kwani wananchi wote mijini na vijijini ukiwasikiliza wote wanadai hawataki Wabunge wa Dar es Salaam wa Mjini wanasema wabunge wa mbezi masaki na dodoma.

MWL.GERALD MUHILE .

:-Huyu pia sio mkongwe au ukipenda mzoefu kwenye siasa kwa mantiki ya kwamba sheria na taratibu za nchi haziwapi nafasi wafanyakazi wa umma kujihusisha na siasa moja kwa moja lakini Muhile ni mtu wa watu kwa kutumia fursa ya nafasi yake ya ualimu anabaki na mtaji mkubwa wa wapiga kura yeye amekua ,Makamu mkuu wa shule ya Kabanga Sekondari ,Mkuu wa shule Mugoma,Mkuu wa shule Lukole na sasa Afisa taaluma wa Idara ya Sekondari wilaya ya Ngara.

Nafasi hizi zote zinampa kura ya turufu kwa wapiga kura wengi kama tu alizitumia vizuri,hofu yangu ni je? chama kinamkubali ananafasi  gani ndani ya chama kiwilaya na kitaifa waweza kujiuliza kwa nini hii iwe hofu yangu kubwa,hii ni kwa sababu uzoefu unaonesha baada ya kura za maoni chama cha Mapinduzi hufanya CHAGUO  kiitikadi kwa maslahi ya chama chao na hii ni sawa kwani ndio utaratibu waliojiwekea.

Ndugu Muhile yeye hana kikwazo cha ukazi hii inamuongezea nafasi endapo chama kitampitisha.

DR.PITTER BUJARI (CHADEMA).

:-Huyu pia sio mkongwe kwenye siasa kwa mantiki ileile kwamba sheria na taratibu havitoi nafasi kwa wafanyakazi wa umma kujihusisha na siasa moja kwa moja lakini kama atagombea itakua ni mara yake ya pili na hii inampa fursa ya uzoefu kwenye siasa za Ngara.

Dr. Bujari anatajwa kisiasa kuwa kipenzi cha watu na kazi yake imempa fursa ya mahusiano na wananchi wa pande zote bugufi na bushubi.

Anatajwa kuwa mtu wa kwanza kuingiza ARV Ngara na mradi wake wa mbuzi kwa kata masikini unampa nafasi ya dhahabu kwenye mbio hizi za ubunge, ananafasi ndani ya chama na hilo nalo linampunguzia presha yeye kama mpinzani hafungwi sana na kigezo cha utayari wa milango ya serikali kumfungukia anachohitaji ni kibali cha wananchi tu,….’’ hofu yangu ni Je wananchi wa ngara wako tayari au wameandaliwa kuzipokea siasa za upinzani?

Hofu inakuwa kubwa zaidi kufuatia uchaguzi wa serikali za mitaa, Dr.Bujari hakufanya vizuri kwao jabo bado ana nafasi jimboni na kwa maoni yangu ukiniuliza atatoa ushindani mkubwa sana .

MWL.HERENA ADRIANI AU MAMA HERENA.

:-Huyu nae anatajwa kugombea ,na ni mwanasiasa mkongwe na mzoefu .
Amekua Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ngara kwa mafanikio makubwa na hii ni karata yake namba moja ndani ya chama.

Pili ni mwanamke miongoni mwa wagombea wote wanaotajwa KUWA NA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015.

Mambo haya mawili yanampa nafasi kubwa ndani ya chama chake kuliko wenzake kuhusu hoja ya milango ya serikali kufunguka mbele yake hilo halina shaka kwani rekodi yake akiwa Mwenyekiti ni ya kuheshimiwa hasa ukizingatia sera isiyio rasimi na wazi ya "usisi" na "uwenzetu" ndani ya CCM lakini pia Herena ni Mkurugenzi wa shure mbili Rhec Primary na Rhec Sekondari.

Kwake hii ni karata ya turufu kwani shule hizo zinakusanya wanafunzi kutoka pande zote za Ngara na hii inamuondolea kikwazo cha kuvuka mto na kumpa mtaji wa kura za pande zote mbili 

Herena kama alivyo Gashaza na Muhile kikwazo cha ukazi kwao sio tatizo ,hapa Herena anachowashinda wenzake wote ndani ya CCM ni moja kukubalika ndani ya chama Ngazi ya wilaya na taifa, hii inampa fursa ikiwa chama kitaamua kufanya uchaguzi wa mezani jina lake lina asilimia 80 za kupitishwa, hii ni kwa sababu ndani ya chama miongoni mwa wagombea yeye ni mwana CCM haswa na pili ana mtaji wa kura pande zote mbili bushubi na bughufi, bushubi kwa maana ya uzawa, uwekezaji wa shule na bughufi kwa maana ya nafasi yake ya Mwenyekiti mstaafu na hivyo basi ukiniuliza kwa maoni yangu mgombea mweye nafasi kubwa ndani ya CCM ni Mama Herena.

NB:-Wengine wanaotajwa kugombea Ubunge Jimbo la Ngara ni pamoja na Bw.Spirian Muhelanyi,Mhadhiri chuo Kikuu UDOM,Bw.Sengati,Mjumbe wa NEC Bw.Issa Samma,Mhandisi wa Barabara mkoani Arusha Bw.Kakoko.

IMEANDALIWA NA 

Mwl. Mwl Venant Vediani

Mwananchi wa kawaida asiye fungamana na upande wowote

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad