Serikali nchini
Tanzania imezipiga marufuku kitendo cha shule binafsi nchini kuwafukuza ama
kuwasitishia masomo wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani na kwamba shule zote
zitakazokiuka agizo hilo zitachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufutiwa
usajili huku ikiongeza kuwa kuanzia mwaka 2016 itaanza kutoa elimu bure kuanzia
shule ya msingi hadi kidato cha nne.
Onyo hilo la
serikali kwa wamiliki wa shule binafsi za serikali limetolewa na Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi Bungeni mjini Dodoma Shukuru Kawambwa,katika kikao cha
kwanza cha mkutano wa 18 ulianza Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu
kutokana na swali la msingi la Mh Conchesta Rwamlaza ambapo Waziri huyo amesema
ni marufuku kwa mameneja na wamiliki wa shule binafsi za sekondari kukaririsha,
kuhamisha ama kuwafukuza shule wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani wa shule
husika kwa kuwa kiwango cha ufaulu kilichowekwa na serikali ni wastani wa
asilimia 30.
Aidha mbunge
wa handeni Dr Henry Shekifu ameitaka serikali kutoa tamko la lini itaanza kutoa
elimu bila ya kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne ili kuwawezesha
watoto wote wa Tanzania kupata elimu ambapo serikali imesema utekelezaji wake
utaanza mwakani.
Awali kabla
ya kuanza kwa shughuli za Bunge,Spika wa bunge hilo Mh Anne Makinda amemwapisha
mwanasheria mkuu mpya wa serikali Ndugu George Mcheche Masaju.
Mara baada
ya kuapishwa nje ya Bunge akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu mswaada
wa sheria ya Mahakama ya kadhi ambao umeanza kuibua mawazo kinzani kwa baadhi
ya viongozi wa dini hasa wa kikristo, Ndugu Masaju amesema wamepitia kwa
umakini mswaada huo na kwamba hauna athari zozote kwa mtu, vikundi vya dini na
taifa kwa ujumla na hautaingilia mambo yanaayosimamiwa na serikali ikiwemo
makosa ya jinai na taifa litaendelea kuwa wamoja.
UNGANANASI KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Wednesday, January 28, 2015
Home
SIASA
SOMA TAMKO HILI:-Marufuku Shule Binafsi Nchini Tanzania kuwafukuza Wanafunzi Wasiofikisha Wastani.
SOMA TAMKO HILI:-Marufuku Shule Binafsi Nchini Tanzania kuwafukuza Wanafunzi Wasiofikisha Wastani.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment