![]() |
Baadhi ya waadishi wa habari wakiwa katika
kutano huo.
NA CHALILA KIBUDA ,GLOBU YA JAMII DAR Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia Bilioni 293 kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mwaka huu ikiwa ni lengo kukuza demokrasia nchini. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo ,Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema wamejipanga kuhakisha watu wenye sifa za kupiga kura wanajiandikisha ili waweze kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa pamoja na kupiga kura ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu. Lubuva alisema kuwa suala la kuwepo wanajeshi katika uchaguzi , wataangalia jinsi gani ya kufanya na kazi ya ulinzi ibaki mikononi mwa jeshi la polisi. ‘’Suala la ulinzi wa jeshi tuliweke na kuangalia jinsi gani tutafanya katika kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa amani na usalama wa mali bila kuwa na hofu ya watu wanaowalinda’’alisema Jaji Mstaafu Damian Lubuva. Aidha alisema uandikishaji wa majaribio, utambuzi wa alama ya mpiga kura kwa kifaa cha BVR ulikwenda vizuri na mapungufu yaliyojitokeza wataendelea kuboresha ili kila mtanzania aweze kujiandikisha na kupiga kura. Alisema uandikishaji wa kanda ya kwanza utaanza Februari 16 hadi Machi 15 ambapo hakutaja mikoa gani itaanza hivyo wanaandaa orodha ya mikoa na kanda katika jinsi ambavyo daftari la kudumu la mpiga litavyoweza kupita kuandikisha.
UNGANANASI KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Friday, January 02, 2015

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TANZANIA(NEC) :-Kutumia Bilioni 293 Kuandikisha Wapiga Kura.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment