LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Januari 28,2015 Simba SC yachapwa na Mbeya City.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 28, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Januari 28,2015 Simba SC yachapwa na Mbeya City..

Simba SC wakimenyana na Mbeya City katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo januari 28,2015  kwenye Mchezo wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara.

 Simba SC imeendelea kupoteza michezo yake hasa ya nyumbani baada ya leo Januari 28,2015 kukubali tena kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imepigwa muda mfupi uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Mashabiki kushuhudia Simba SC wakikosa penati dakika za lala salama baada ya kugonga mwamba wa juu huku magoli ya mchezo huo yakifungwa kwa Simba SC na Ibrahim Salum Hajib na Mbeya City kwa Penati ya Yusuf Abdallah na Hamad Kibopile .

Simba SC hivi karibuni ilipoteza mechi yake ya nyumbani baada ya kupigwa na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaa, kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC .

Matokeo hayo ya kufungwa yanaiacha Simba SC ikiwa na alama 13 baada ya mechi 11 huku Mbeya City ikifikisha alama 15 kwa mechi 11 pia.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad