|
Ndugu na majirani wakiwa na makamanda wa Polisi
eneo la tukio.
“Cha
ajabu alikuwa akizuia watu kuingia ndani. Kumbe alishajua
kinachoendelea na akiruhusu sisi kuingia nini kitatokea.“Hata hivyo majirani
kwa kushirikiana na mimi na baba wa mmoja wa watoto waliouawa (Sudi Mrisho),
Mrisho Abdallah tulimshika kwa nguvu Zuhura, watu wakaingia.”
WAKUTA
MASHIMO MAWILI
“Tulipofika, tukabaini mashimo mawili aliyokuwa amewafukia watoto wake. Shimo
moja sebuleni, jingine chumbani. Tuliwapa taarifa polisi wakafika haraka sana.
Mashimo yalipofukuliwa, watoto walikutwa ndani ya mifuko miwli ya sandarusi.
Inauma sana. ”
MTUHUMIWA
AZUNGUMZA NA WANAHABARI
Amani lilibahatika kuzungumza na mwanamke huyo katika mahojiano mafupi akiwa
chumbani muda mfupi kabla ya polisi kufika.Amani: “Hivi Zuhura, ni kwanini
umeamua kuwaua watoto wako wa kuwazaa?”
Zuhura: “Nani? Mimi sijui, we (mwandishi) ndiyo unajua.”Amani: “Watoto wako
wako wapi?”
Zuhura: “Nani? Wako wapi kwani?”
KILICHOONEKANA
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema, Zuhura licha ya kuonekana hana wasiwasi
wowote, lakini pia aliashiria kujitoa ufahamu ili atafsirike kwamba hakuwa na
akili timamu.
KUMBUKUMBU
MBAYA
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa majirani zinadai kuwa, mwaka 2013, Zuhura
alidaiwa kumsababishia kifo mtoto wake mchanga wa kiume kufuatia
kumzidishia dozi ya malaria wakati alipokuwa akiumwa.
KAMANDA
WA POLISI
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Juma Bwire ilikiri kutokea
kwa tukio hilo.
Afande Bwire alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi
kukamilika.
Chanzo :-GPL.
|
No comments:
Post a Comment