Wafuasi 30
wa Chama Cha Wananchi (CUF) akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi
na Bunge, Shaweji Mketo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Abdul Kambaya wamefikishwa
kortini kwa tuhuma za mashtaka matatu likiwemo la kufanya mkusanyiko usio
halali, ambapo wameshindwa kutimiza masharti na dhamana na kupelekwa rumande.
Wakili wa
serikali Joseph Maugo amedai mbele ya hakimu Emilius Mchauro wa mahakama ya
hakimu mkazi kisutu, jijini Dar es Salaam kuwa washtakiwa wanatuhuma kwa
mashtaka matatu ambapo shitaka la kwanza linawakabili washtakiwa wote ambao
wanatuhumiwa kula njama ya kufanya uhalifu. Shtaka la pili linawakabili
washtakiwa 28 ambao wanatuhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali.
Imedaiwa
kuwa walifanya mkusanyiko huo Januari 27 mwaka huu, wakiwa katika ofisi ya CUF
iliyopo karibu na hospitali ya Temeke bila uhalali wowote walifanya mkusanyiko
wa nia ya kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Zakhiem, Mbagala, Dar es
Salaam.
Katika
shtaka la tatu pia linawakabili washtakiwa 28, wanadaiwa kufanya mgomo baada ya
katazo halali ambapo washtakiwa bila kujali tangazo lililotolewa na jeshi la
polisi la kutokufanya maandamano wao walikaidi wote wamekana kuhusika na tukio
hilo huku wakili Maugo akidai upelelezi bado na pia kisheria mashtaka yao yana
dhamana.
Mchauro
amesema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana wanatakiwa wasaini dhamana ya sh.
100,000 na mdhamini mmoja wa kuaminika, lakini washtakiwa walishindwa kutimiza
masharti ya dhamana na kurudishwa rumande.
Washtakiwa
hao watarudishwa mahakamani Leo Januari 30,2015 ili kuangalia kama wametimiza masharti
ya dhamana, baada ya barua za wadhamini kwenda kuhakikiwa na upande wa
mashtaka.
Nje ya
mahakama hiyo kundi la wafuasi wa chama hicho walionekana wakihangaika huku na
kule wakitaka kuwadhamini ndugu zao bila mafanikio na baada ya zoezi hilo
kukwama walisubiri kuona wafuasi hao wanavyoondoka mahamani hapo ambapo
waliwasindikiza kwa nyimbo za chama hicho.
|
No comments:
Post a Comment