Sijui
tukamate wapi baina ya kauli tofauti mbili au tatu za jeshi la polisi TZ kuhusu
kadhia ya kupigwa mabomu ya machozi wafuasi wa CUF na kiongozi wao,
Prof.Lipumba. Au kwa kuparangaya kiswahili niseme ‘tofauti ya kauli au kauli
tofauti’. Ipi bora kwetu kuifahamu zaidi!
Awali
tumeambiwa kama ifuatavyo – soma hapa chini:-Naibu
kamishna wa Polisi Kanda hiyo, Simon Siro jana alisema: “Tumewakamata na
tunaendelea kuwahoji… tulipewa taarifa ya maandamano hayo na viongozi wa chama
na tuliwaandikia barua ya kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.
“Sababu
kubwa ya kuzuia maandamano hayo yasifanyike ni kuwa mwaka 2001 yalifanyika
maandamano batili yaliyosababisha baadhi ya polisi na wananchi kufa.
“Polisi
tumeona, tukiruhusu maandamano haya, kuna uwezekano wa kutokea fujo kama
ilivyotokea mwaka 2001.”
Alisema
sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo ni kwamba hivi karibuni walikamatwa
watu wanaojihusisha na ugaidi na kwamba kutokana na mazingira hayo polisi
inazuia mikusanyiko mikubwa kwa kuhofia kutokea mambo mabaya.
Jana kauli
nyengine ya polisi inasema kuwa ‘hofu kubwa ilikuwa silaha zilizoibiwa
Ikwiriri, Rufiji’. Haya wpai na wapi, where is the connection! Huu ni dhahiri
uwongo wa kimacho macho – na kama bunge lina ukweli na liko serious, basi
wahusika laizma wawajibike maana hii kisheria ni kusema uwongo.
3. Ukipima
utaona kuwa polisi limesema uwongo. Na ukisoma ‘between the lines’ utaona kuwa
walipanga kufanya hujuma hii kwa visingizio tofauti – ‘ugaidi’, mara ‘silaha
zilizoibiwa rufiji’, mara aliuliwa polisi 2001 Pemba — yote haya hayana
mashiko. Serikali siku zote inatakiwa iwe serious, na hata kama inasema uwongo
basi uwe ni uwongo wa ‘kweli’, na sio ‘uwongo’ bin uwongo bila mchuzi! au ndio
‘Wapigwe tu, na wpaigaji wapo’ — ahsante mizengo Pinda.
Source: Mzalendo
|
No comments:
Post a Comment