KUTOKA BUNGENI:-Soma Wabunge walichokisema kuhusu kudhalilishwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF na Tamko la LHRC . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 30, 2015

KUTOKA BUNGENI:-Soma Wabunge walichokisema kuhusu kudhalilishwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF na Tamko la LHRC .

Serikali imetakiwa kubadili mfumo wa utendaji Kazi  wa Jeshi la Polisi nchini kutokana na kuwa na mifumo ya kikoloni na ukandamizaji jambo linalolifanya Jeshi hilo kutenda shughuli zake kwa kukiuka haki za binadamu.


Hayo yamesemwa Bungeni mjini dodoma jana Januari 29,2015 na baadhi ya Wabunge wakati wakichanga mjadala wa hoja ya dharura iliyowasilishwa Bungeni na Mh. James Mbatia kufuatia tukio la kupigwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba Januari 27,2015.

Aidha baadhi ya Wabunge wamemtaka Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.Mizengo Pinda kuliomba Bunge radhi pamoja na watanzania wote na kisha kufuta kauli yake aliyoitoa bungeni inayodaiwa kuhamasisha Polisi kupiga raia sambamba na Waziri wa mambo ya ndani Mh. Mathias  Chikawe kujiuzulu nafasi yake.

Pia wamependekeza kuwajibishwa kwa baadhi ya polisi waandamizi walioshiriki katika matukio mbalimbali yaliyosababisha mauaji na majeraha kwa wananchi badala ya kuwapandisha vyeo pamoja na kuweka mifumo itakayolifanya jeshi hilo kuwa huru badala ya kuwa jeshi la kupokea maagizo.

Katika Hatua nyingine , Kituo cha sheria na haki za binadamu kimelaani kitendo cha jeshi la polisi kumpiga na kumdhalilisha mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF kuwa hakivumiliki na kina lengo la kudhoofisha demokrasia na uhuru wa kikatiba katika kufanya maandamano.

Akitoa tamko hilo lililokuwa katika sehemu ya maazimio katika kongamano la kujadili mapungufu ya katiba pendekezwa kwa wahariri wa vyombo vya habari, asasi za kiraia na wanazuoni, mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi. Hellen Kijo Bisimba amesema,''-Jeshi la polisi litakakiwa kijitazama upya katika kutekeleza wajibu wao wa kulinda raia na mali zao vionginevyo wanaendelera kujenga chuki baina yao na wananchi kwa hila za kisiasa badala ya kuwa kimbilio la raia.
Katika mjadala wa mapungufu ya katiba pendekezwa, Profesa Peter Maina pamoja na kuunga mkono UKAWA kujiondoa katika mchakato, alizungumzia udhaifu kuanzia utashi wa kisiasa kwa chama tawala CCM kutotaka katiba mpya kwa kauli za viongozi wake, mchakato wa sheria ya mabadiliko ya katiba na bunge maalum kukosa maridhiano na mjadala kuendeshwa kwa haraka na usiri wa kiitikadi akieleza kuwa ni hatari kwa usalama wa nchi kwa kufanya maamuzi mazito wakitumia njia nyepesi.

Aidha katika mada iliyowasilishwa na aliyekuwa mjumbe wa bunge la katiba Bw. Hafley Polepole pamoja na kueleza katiba pendekezwa kuwa na papungufu mengi ya kiuandishi na kisanifu amesema ni aibu kwa Tanzania yenye wasomi kuandika katiba kama hiyo huku akieleza sheria ya mabadiliko ya katiba kuwa nje ya muda wa kura ya maoni kutokana kutoboreshwa kwa daftari hadi sasa inayofuatiwa na siku stini za elimu kwa wapiga kura kabla ya muda wa kampein.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad