MAPINDUZI CUP 2015:-Soma Matokeo ya Yanga SC leo Januari 04,2015 pamoja na Azam FC ndani..' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 04, 2015

MAPINDUZI CUP 2015:-Soma Matokeo ya Yanga SC leo Januari 04,2015 pamoja na Azam FC ndani..'

Mliberia Kper Sherman alifunga bao la pili kwneye mchezo huu na bao lake la pili kwenye kombe la Mapinduzi 2015.

Yanga SC leo Januari 04,2015,wameingia  hatua ya Robo Fainali ya Mashindano ya Mapinduzi Cup 2015 ,yanayofanyika huko Visiwani Zanzibar baada ya kuitandika Polisi ya Zanzibar Bao 4-0 kwenye Mechi ya Kundi A.

Ushindi huu ni wa pili kwa Yanga SC kwenye Kundi lao baada ya kuichapa Taifa ya Jang’ombe Bao 4-0 katika Mechi yao ya kwanza na sasa wanaongoza Kundi A wakiwa na Pointi 6. 


Hadi Mapumziko Yanga walikuwa 2-0 mbele kwa Bao za Mchezaji wa Brazil Coutinho na yule wa Liberia Kpah Sherman.

Kipindi cha Pili Yanga walipiga Bao nyingine 2 kupitia Coutinho na Simon Msuva.

Nao Azam FC imepata ushindi wa kwanza katika Kombe la Mapinduzi, baada ya kuwalaza mabingwa wa Ligi Kuu visiwani Zanzibar , KMKM 1-0 ,mchezo ukipigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Shukrani kwake, beki Shomary Kapombe aliyesababisha bao hilo pekee dakika ya 18, na kuifanya Azam FC sasa ifikishe pointi nne baada ya awali kutoa sare ya 2-2 na mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda.

Bao hilo lililfungwa na Khamis Ali ‘Chichi’, Nahodha wa KMKM aliyejifunga kwa kichwa akijaribu kuokoa shuti la Shomary Kapombe alilopiga kutoka umbali wa mita 25.

KCCA sasa inaongoza Kundi B kwa pointi zake nne, sawa na Azam FC, lakini yenyewe ina wastani mzuri wa mabao baada ya jioni ya leo kuifunga Mtende mabao 3-0.

Mechi nyingine zilizochezwa leo, Taifa ya Jang’ombe imeilaza 1-0 Shaba Uwanja wa Mao dze Tung, wakati Yanga SC imeifunga Polisi mabao 4-0, mechi zote za Kundi A.

Michuano hiyo, itaendelea kesho kwa mechi za mwisho za Kundi C, Mtibwa Sugar wakimenyana na Mafunzo Saa 10:00 jioni na baadaye Simba SC na JKU Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Jumatatu Januari 5,2015.

1500 Mtibwa v Mafunzo

2015 Simba v JKU

Jumanne Januari 6,2015.

1500 KCCA v KMKM

1500 Polisi v Taifa ya Jang’ombe [Uwanja wa Mao]

1700 Azam FC v Mtende

2015 Yanga v Shaba

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad