Cristiano
Ronaldo akiifungia Real Madrid bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati leo January 04,2015 kwenye mechi ya Ligi kuu Hispania.
Mabingwa wa
ulaya ,Real Madrid hii leo January 4, 2015,(jumapili) wameuanza vibaya mwaka
2015 baada ya kukubali kipigo cha 2-1 toka kwa Valencia katika mchezo wao wa 17
wa ligi kuu ya Hispania 2014/2015 na kufanya zile mbio za Mechi 22 za Real
Madrid bila kufungwa katika Mechi rasmi za Mashindano.
Mchezo huo
wa Ligi uliopigwa kwenye uwanja wa
nyumbani wa Valencia Estadio Mestalla, Cristiano
Ronaldo aliipa Real Bao la kuongoza wa Penati ya Dakika ya 14 lakini Valencia
wakapiga Bao 2 Kipindi cha Pili kupitia Antonio Barragan na Nicolas Otamendi
kuwapa Bao la ushindi.
Matokeo hayo
yamewabakisha Real Pointi 1 mbele ya Barcelona ambao wanaweza kutwaa uongozi
wakiifunga Real Sociedad baadae usiku wa leo January 4, 2015, ingawa Barcelona
watakuwa wamecheza Mechi 1 zaidi.
|
No comments:
Post a Comment