AFCON 2015:-Baada ya Guinea kupita kwa kamari sasa hii ndio Ratiba ya Robo Fainali kuwavaa Ghana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 30, 2015

AFCON 2015:-Baada ya Guinea kupita kwa kamari sasa hii ndio Ratiba ya Robo Fainali kuwavaa Ghana.

Timu ya Taifa ya Guinea imeshinda kamari iliyopigwa kupata timu ya pili ya kundi D inayofuzu robo fainali ya kombe la Mataifa ya Africa, Afcon 2015 na sasa itacheza na Ghana katika hatua hiyo.


Sheria ya CAF kipengele cha 74 kimetumika kuamua mshindi baina ya Mali na Guinea ambao walimaliza wakifanana kwa kila kitu.

Sheria hiyo pia inatumika na shirikisho la soka Duniani FIFA.

Timu zikifungana kila kitu basi hufanywa Bahati Nasibu ili kupata Mshindi na hii ni mara ya kwanza kwa Mshindi kupatikana kwa njia hii kwenye Mashindano haya tangu 1988 wakati Algeria iliposhinda Tombola hiyo na kuibwaga Ivory Coast.

Mbele ya Kamati ya Matayarisho ya CAF, Rais wa Mali, Boubacar Diarra, ndio alikuwa wa kwanza kutoa Kimpira toka kwenye Chungu chenye Jina la Nchi yake na hivyo kuthibitisha wamemaliza Kundi D wakiwa Nafasi ya 3 na akaja Amara Dabo, Mkurugenzi wa Fedha wa Wizara ya Fedha ya Guinea, ambae aliokota Mpira wa Pili uliobakia ambao ulithibitisha Guinea wamemaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Washindi wa Kundi D, Ivory Coast na hivyo kusonga Robo Fainali.

AFCON 2015 RATIBA.

**Saa za Bongo

ROBO FAINALI

Jumamosi Januari 31,2015.

1900 Congo v Congo DR Kundi B [Estadio de Bata]=RF1 
    
2200 Tunisia v Equatorial Guinea [Estadio de Bata]=RF2

Jumapili Februari 1,2015.

1900 Ghana v Guinea [Estadio de Mongomo]=RF3   

2200 Ivory Coast v Algeria [Nuevo Estadio de Malabo]=RF4 

NUSU FAINALI

Jumatano Februari 4,2015.

2200 RF 1 v RF4 [Estadio de Bata]=NF1

Alhamisi Februari 5,2015.

2200 RF2 v RF3 [Nuevo Estadio de Malabo]=NF2 
     
MSHINDI WA 3

Jumamosi Februari 7,2015.

2100 Aliefungwa NF1 v Aliefungwa NF2 [Nuevo Estadio de Malabo]

FAINALI

Jumapili Februari 8,2015.

2200 Mshindi NF1 v Mshindi NF2 [Estadio de Bata]    


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad