KUTOKA BUNGENI DODOMA:-Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote wanaohusika na upotevu wa fedha za Serikali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 30, 2015

KUTOKA BUNGENI DODOMA:-Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote wanaohusika na upotevu wa fedha za Serikali.

Bunge limechachamaa na kutaka serikali ianze kuchukua hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwakamata, kuwashtaki na kuwafilisi wale wote wanaohusika katika ubadhirifu na upotevu wa fedha za serikali kutokana na kukosa uzalendo na uwajibikaji badala ya kila mwaka bunge kupokea ripoti ya ubadhirifu unaosababishia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi na kwamba kujiuzulu ama kufukuzwa kazi pekee si suluhisho ili kuwa na taifa lenye nidhamu katika matumizi ya fedha za umma.


Bunge limepata fursa ya kuzijadili taarifa za kamati ya bunge ya hesabu za serikali ambayo taarifa yake inaonesha kuwa zaidi ya shilingi bilioni 100 zimekwepwa kulipwa na makampuni mbalimbali kwa kivuli cha misamaha ya kodi na takribani bilioni 8 nazo zikipotea baada ya mamlaka ya bandari kufanya manunuzi ya dharura bila kibali cha mlipaji mkuu wa serikali jambo liliwafaanya baadhi ya wabunge kugeuka mbogo.

Hata hivyo wakati majadiliano yakiendelea kukaibuka mabishano ya kisheria dhidi ya mh Tundu Lissu na mwanasheria mkuu wa serikali Ndg George Mcheche Masaju baada Mh Lisu kutaka rais awawajibishe baadhi ya majaji waliohusika katika sakata la Tegeta Escrow kwa kuwa katiba inampa mamlaka huku ndg Masaju akiliambia bunge tume ya utumishi wa mahakama kwa mujibu wa katiba ndio inapaswa kumshauri rais juu ya masuala ya nidhamu za majaji.

Kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kuepuka kuingilia mihimili mingine hasa mahakama baaadhi ya wabunge wameonesha kutoridhika na hoja hiyo kutokana na wabunge kuzuiwa kulijadili sakata la uda kutokana na taarifa za uwepo wa kesi kadha wa kadha mahakamani zinazohusu uda  baada ya mwanasheria mkuu wa serikali kushauri kutojadiliwa bungeni kutokana na kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa kuitaka serikali kutoa maelezo bungeni endapo ni kweli hisa za uda zimeuzwa kwa kampuni binafsi ya simon group limited ama la.

Mara baada ya muongozo huo mwenyekiti Mh Musa Azan Zungu akaitaka kamati uongozi ya bunge kukutana ili kulijadili suala hilo kwa madai kuwa kuna mambo yako mahakamani na mengine hayapo mahakamani lakini bunge linakosa fursa ya kuyajadili.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad