Vyanzo
vingine vya habari vimeeleza kuwapo pia kwa ajenda ya hali ya siasa
inayohusishwa na harakati za urais, hususan kwa vigogo wanaopishana kusaka
nafasi hiyo na wale waliotajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Kamati Kuu
inatarajia kutumia vikao hivyo kuangalia namna ya kupata wagombea
watakaokubalika kwa wananchi kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha urais, wabunge
na madiwani.
Akiwa katika
ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kuipa CCM ushindi kwenye Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa mkoani Tanga, Kinana alisema chama hicho kitafanya kikao hicho kwa
lengo pia la kupitia masuala mbalimbali yanayokihusu.
Alisema
salamu za CCM kwa Watanzania kwa mwaka huu ni ahadi ya kuweka mkazo katika
maadili kwa viongozi wake na itafanya tathimini kwa lengo la kujipanga kwa
Uchaguzi Mkuu.
Alipoulizwa
kuhusu ajenda katika vikao hivyo wiki iliyopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye alikuja juu na kusema hakuna kitu kama hicho. “Hata mkiiandika
vibaya CCM itashinda tu,” alisema hivi karibuni.
Vigogo
waliopewa onyo na CCM ni pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba na mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na
Frederick Sumaye.
Wengine ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wasira na aliyewahi kuwa
Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na
waziri waliokumbwa na kashfa ya escrow ni Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Habari
Na:-Gazeti la Mwananchi Januari 12,2015.
|
No comments:
Post a Comment