KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM 2015 ZANZIBAR:-‘Hatufukuzi mgombea urais CCM’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 14, 2015

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM 2015 ZANZIBAR:-‘Hatufukuzi mgombea urais CCM’

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM , mjini Unguja , Zanzibar jana Januari 13,2015.  Kushoto ni Makamu wake (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.

Wakati Kamati Kuu ya chama tawala, CCM ikimaliza vikao vyake mjini Zanzibar, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana amesema mambo mengi yanayozungumzwa kuhusu baadhi ya wanachama wanaotajwa kuwania urais hayana ukweli, wala hakuna atakayefukuzwa uanachama.

Kinana aliyasema hayo jana Januari 13,2015, kuhusu mambo yaliyojitokeza kwa wagombea wa nafasi za urais kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu, Oktoba,2015.

Kamati Kuu ya CCM hadi jana  jioni ilikuwa ikiendelea na kikao chake kwenye ofisi kuu ya chama, Kisiwandui, Zanzibar.

Kauli ya Kinana imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono kuwa baadhi ya makada waliojitokeza kutangaza ama kuonyesha nia kuutaka urais watachukuliwa hatua, zikiwamo kutimuliwa.

“Mambo yanayozungumzwa ni mengi kuwa baadhi ya wagombea majina yao yatakatwa. Hayo ni majungu ya kisiasa, yamelenga kuwachokoza viongozi na chama ili wapate cha kusema.

Chama kina utaratibu na uamuzi unaofanyika kwa vikao maalumu, hizi ni propaganda, ni uchokozi kwa chama chetu,” alisema Kinana.
Wakati Kinana akijaribu kuwaondoa hofu vigogo wanaowania nafasi hiyo, tayari wagombea hao wamepiga kambi mjini Zanzibar, baadhi yao wakiendesha kampeni za chini chini, tangu kumalizika kwa sherehe za Mapinduzi visiwani hapa Januari 12,2015.

Wagombea hao wamekuwa wakipishana kuingia visiwani na kukutana na baadhi ya wajumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM na mkutano mkuu kila upande ukijiimarisha kisiasa kabla ya mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia chama hicho Mei mwaka huu.

Vikumbo mitaani.

Katika hoteli kadhaa mjini hapa baadhi ya makada wamekuwa wakipigana vikumbo ikiwa ni hatua ya kuweka mikakati ya kutengeneza mazingira, hasa ya kukubalika katika chama hicho.

Hata hivyo, tofauti na vikao vingine vya chama hicho tawala, idadi ya wapambe wa makundi yanayotajwa kuwania urais waliofika mjini Zanzibar imekuwa ni ndogo.

Makada kadhaa wanatajwa kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Uhusiano na Uratibu) Stephen Wasira, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangala, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Tibaijuka akosekana CC.

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anne Tibaijuka ni mmoja kati ya wajumbe wawili walioshindwa kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Kisiwandui.GONGA HAPA KUSOMA ZAIDI TAARIFA HII.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad