IVO MAPUNDA HAKUNAGA:-Aipa Simba SC Kombe la Mapinuduzi 2015..Tazama Picha hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 14, 2015

IVO MAPUNDA HAKUNAGA:-Aipa Simba SC Kombe la Mapinuduzi 2015..Tazama Picha hapa.

Simba SC walikabidhiwa Kombe la Mapinduzi 2015 pamoja na Shilingi Milioni 10 kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohammed Shein na aliepokea zawadi hizo alikuwa Nahodha wa Simba, Hassan Isihaka.

Wachezaji wa Simba wakishangilia na kombe la Mapinduzi walibeba usiku wa jana Januari 13,2015, uwanja wa Amaan Zanzibar.

Wekundu  wa Msimbazi Simba chini ya kocha mpya, Goran Kopunovic wametwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi 2015 kufuatia kuifunga Mtibwa Sugar penalti 4-3 katika mechi ya fainali iliyopigwa usiku wa jana kwenye uwanja wa Amaan, Mjini Zanzibar.

Bingwa wa mashindano hayo alilazimika kupatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu pacha ya bila kufungana.

Kuhakikisha wanatwaa Ubingwa, Simba walimtoa Peter Manyika katika dakika ya 90 na nafasi yake kuchukuliwa na Ivo Mapunda.

Mapunda ni mzoefu wa kudaka penalti hakuwaangusha katika mapigo hayo.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, hakuna timu iliyoona lango la mwenzako.
 
Baada ya hapo mikwaju ya penalti ilifuata na Simba ndio walikuwa wa kwanza kupiga.
 
Waliofunga Penalti kwa upande wa Simba ni Awadh Juma, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Danny Sserunkuma wakati Shaaban Kisiga alikosa.
 
Waliofunga kwa upande wa Mtibwa Sugar ni Ally Lundenga, Shaaban Nditi, , Ramadhan Kichuya, wakati Ibrahim Rajab na Vicent Barnabas walikosa penalti hizo.

Mkombozi  wa Simba SC katika mechi ya fainali ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyopigwa uwanja wa Amaan Jana Januari 13,2015, Mjini Zanzibar, Ivo Philip Mapundo amejawa na furaha kubwa baada ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa kufuatia kudaka penalti ya Vicent Barnabas iliyowapa ushindi na kuwafanya Wachezaji wa Simba walimbeba shujaa wao .

Simba walikabidhiwa Kombe la Mapinduzi pamoja na Shilingi Milioni 10 kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohammed Shein na aliepokea zawadi hizo alikuwa Nahodha wa Simba, Hassan Isihaka.
Nahodha wa Simba, Hassan Suleiman Isihaka alikosa cha kuzungumza baada ya kuiongoza Simba kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi 2015 katika mechi ya fainali iliyomalizika kwa suluhu ya bila kufungana na hatimaye Simba kuibuka washindi kwa penalti 4-3, Isihaka alicheza safu ya ulinzi akisaidiana na Juuko Mursheed, huku kushoto akikaa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kulia Hassan Ramadhani Kessy.

Kocha mkuu wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic amesema kipa wake Ivo Mapunda ni shujaa mkubwa na uzoefu wake unaisaidia timu.

Okwi (kushoto)  alitolewa dakika ya 75 na nafasi yake kuchuliwa na Awadh Juma (kulia)

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad