|
Chama cha
ACT-Tanzania kimemsimamisha aliyekuwa Mwenyekiti wake wa muda, Kadawi Limbu na
kumwondoa katika nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kutokana na
makosa mbalimbali waliyoyafanya ndani ya chama hicho.
Akitangaza
maazimio ya Chama hicho, yaliyotokana na Mkutano wa Halmashauri Kuu Taifa
uliofanyika Januari 12,2015, Katibu Mkuu wa ACT, Samson Mwigamba (Pichani) alisema uamuzi
huo umefikiwa baada ya wajumbe 57 kati ya 65 sawa na asilimia 87.7
waliohudhuria mkutano huo kupiga kura ya kutokuwa na imani kwa viongozi hao.
Alisema
katika mkutano huo wa pili wa kawaida wa Halmashauri Kuu ya ACT Tanzania pamoja
na mambo mengine, ilipokea na kujadili taarifa mbalimbali na kutoa maamuzi na
maazimio, yakiwemo yanayowahusu viongozi hao.
Mwigamba
alisema kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho, adhabu hiyo itakuwa ya miezi sita
bila kuwasimamisha nafasi za uanachama wao huku wakiruhusiwa kugombea katika
nafasi mbalimbali katika mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaotarajiwa kufanyika
Machi 28 Mwaka huu.
Alitaja
baadhi ya makosa hayo kuwa ni pamoja na kuitisha kikao haramu kinyume cha
Katiba na kuwafukuza wenzao uanachama, kusababisha mtafaruku ndani ya chama
kutokana na vikao hivyo pamoja na kukiuka taratibu zingine.
Chanzo:-Habari
Leo.
|
No comments:
Post a Comment